Wizara ya Mambo ya Nje ya China imesema Jumatatu kuwa mazungumzo ya kibiashara kati yake na Marekani ni vigumu kufanyika katika hali hii ya mvutano unaoendelea.
Maoni hayo yaliyotolewa na msemaji wa wizara hiyo Geng Shuang wakati akiwapa muhtasari waandishi wa habari juu ya hali ya mazungumzo hayo ambao umetolewa siku moja baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kutabiri kuwa kutakuwa na suluhisho katika mvutano uliopo baina ya Marekani na China.
Shuang alikuwa anawaeleza waandishi juu ya ushuru uliowekwa kwa bidhaa zenye thamani ya mabilioni ya Dola za Kimarekani ambapo mataifa hayo mawili yenye uchumi mkubwa kuliko yote duniani wanatishiana kuanzisha ushuru huo kutoka kila upande.
“China itaondosha vikwazo vya kibiashara kwa sababu ni jambo lililo sahihi kulitekeleza,” amesema Trump, bila ya kutoa maelezo ya moja kwa moja juu ya suala hilo.
Amesema: “Ushuru huo utakuwa wamaridhiano kati ya pande mbili na tutafikia makubaliano katika suala la haki miliki. Kuna mustakbali mwema kwa nchi zote mbili!”
Vyovyote itavyokuwa, Trump amesema kuwa yeye na Rais wa China Xi Jinping “wataendelea kuwa marafiki, bila ya kujali nini kimetokea katika mvutano wao wa kibiashara.
Tishio ambalo Washington na Beijing wametupiana katika siku za hivi karibuni limetikisa soko la hisa la biashara, na kuyumbisha mamia ya numbari za mwelekeo wa hisa hizo.
No comments:
Post a Comment