Wednesday, August 23

TABORA

TIGO YAKABIDHI KISIMA CHA MAJI KWA WANANCHI WA KIJIJI CHA USONGELANI WILAYANI URAMBO, TABORA


Mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanry akipampu maji katika kisima cha maji kilichotolewa Msaada na Kampuni ya simu za Mkononi nchini Tigo katika Kijiji cha Usongelani wilayani Urambo mkoani Tabora,Kisima hicho kimegharimu zaidi ya shilingi milioni 18. 
Mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanry akifungua pazia kuashiria uzinduzi rasmi kisima cha maji kilichotolewa Msaada na Kampuni ya simu za Mkononi nchini Tigo katika Kijiji cha Usongelani wilayani Urambo mkoani Tabora. Kisima hicho kimegharimu zaidi ya shilingi milioni 18.
Mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanry akimtwisha ndoo ya maji mmoja kati ya wananchi wa kijiji cha Usongelani ikiwa ni ishara ya kuzindua kisima hicho kilichotolewa msaada na kampuni ya Tigo ambapo kitahudumia wakaazi wa Kijiji cha usongelani na maeneo jirani ikiwa ni hatua muhimu kwa kampuni ya Tigo kurejesha kiasi cha faida kwa wananchi. 

Mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanry (wa pili kushoto walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya simu ya Tigo pamoja na watendaji wa Mkoa huo, baada ya uzinduzi wa kisima kilichotolewa msaada na Tigo wakati wa hafla fupi ya kukabidhi kisima hicho kwa wakaazi wa kijiji cha Usongelani kilichogharimu zaidi ya shilingi milioni 18.

DKT. PHILIP MPANGO ATEMBELEA KIWANDA CHA KUUNGANISHA MATREKTA YA URSUS-KIBAHA


Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (katikati) akiwasili katika kiwanda cha kuunganisha Matrekta ya URSUS-TAMCO, kilichoko Kibaha mkoani Pwani kuangalia kazi ya uunganishaji matrekta zaidi ya 200 pamoja na kusikiliza changamoto zinazoukabili mradi huo.

Na. Benny Mwaipaja-Kibaha

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ametembelea mradi wa kuunganisha matrekta ya Ursus, uliopo Kibaha mkoani Pwani na kusisitiza kuwa Serikali imedhamiria kuendeleza kilimo nchini ili kukuza sekta ya viwanda.

Tayari Matrekta 204 yenye uwezo wa HorsePower 50 yamekwisha unganishwa yakisubiri kuuzwa kwa watumiaji hatua ambayo Dkt. Mpango amesema itaongeza tija katika kilimo na kukuza ajira hususan kwa kundi kubwa la vijana.

Ameahidi pia kuwa Serikali itayafanyiakazi haraka maombi ya Shirika la Maendeleo la Taifa NDC la kutaka kupata kibali cha kuajiri zaidi ya wafanyakazi 90 watakaohusika na mradi huo pamoja na kutoa shehena ya Matrekta 267 yaliyokwama katika Bandari ya Dar es Salaam ili yaweze kuuzwa kwa wananchi kuendeleza kilimo.

 Kwa upande wake, Meneja wa Mradi huo kutoka Shirika la Maendeleo la Taifa-NDC, Mhandisi Adam Mbura, amesema mradi huo utahusisha pia uanzishwaji wa vituo vinane katika kanda mbalimbali kwa ajili kuuza matrekta, zana na vifaa vingine pamoja na  kutoa huduma kwa wateja.

Amesema kuwa kukwamuliwa kwa makontena 64 yaliyokwama bandarini yakiwa na matrekta hayo 267 pamoja na vipuri vya kuunganisha Matrekta hayo pamoja na baadhi yaliyopo katika eneo la Mradi la TAMCO, Kibaha mkoani Pwani, kutawezesha kukamilisha haraka kwa kazi hiyo.

Baadhi ya vijana wanaofanyakazi katika mradi huo wamesema kuwa wamenufaika na ujuzi wanaoupata kutoka kwa wataalamu wa ufundi kutoka nchini Poland na kuahidi kuuendeleza ujuzi huo kwa vijana wenzao ili mradi huo uweze kuwa na manfaa kwa kutatua changamoto mbalimbali za kiufunsi zitakazokuwa zikiwakabili wakulima

Mradi wa kuunganisha Matrekta ya URSUS-TAMCO, Kibaha Mkoani Pwani unafadhiliwa na Serikali ya Poland ambapo kiwanda kikubwa cha kuunganisha matrekta kinatarajiwa kujengwa katika eneo hilo na yatauzwa kwa gharama nafuu, kati ya shilingi milioni 38 hadi milioni 42 kulingana na ukubwa na uwezo wa trekta.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango akiwasha moja ya matrekta yaliyounganishwa katika Mradi wa Kuunganisa Matrekta ya URSUS-TAMCO, uliopo katika eneo la Kibaha mkoani Pwani, alipotembelea mradi huo.
Meneja Mradi wa Kuunganisha Matrekta ya URSUS, Kibaha mkoani Pwani, Mhandisi Adam Mbura, akimweleza Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango, moja ya majembe yaliyounganishwa kupitia mradi huo.
Mafundi pekee wa kike katika Mradi wa Kuunganisha Matrekta ya URSUS katika eneo la Kibaha Mkoani Pwani, Bi. Fatma Abbass (kulia) na Rahabu Japhet wakisikiliza wosia na maelekezo kutoka kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango, (hayupo pichani) alipotembelea Mradi huo.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (aliyevaa tai) akiwa katika picha ya pamoja na vijana mafundi wanaounganisha matrekta katika Mradi wa kuunganisha Matrekta ya URSUS, kilichopo Kibaha mkoani Pwani.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Benny Mwaipaja, (kushoto) akizungumza na Meneja Mradi wa kuunganisha Matrekta ya URSUS, Mhandisi Adam Mbura, (katikati) katika eneo la mradi huo uliopo Kibaha mkoani Pwani ambapo tayari matrekta 204 yameunganishwa katika awamu ya kwanza ya mradi huo ambapo zaidi ya matrekta 2,400 na zana zake yanatarajiwa kuunganishwa, wakati Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango alipofanya ziara kwenye mradi huo.
Sehemu ya matrekta 204 yaliyounganishwa katika Mradi wa Kuunganisha Matrekta ya URSUS-TAMCO, katika eneo la Kibaha mkoani Pwani.

USAILI KWA WALIOOMBA KAZI MFUKO WA PPF KUFANYIWA AGOSTI 28


SERIKALI KUONDOA KABISA MFUMO WA ZAMANI WA MALIPO YA KODI YA ARDHI NCHI NZIMA


Maafisa kutoka Ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Ziwa wakijifunza jinsi ya kutumia Mfumo wa GePG katika malipo ya Kodi ya aedhi.

Na. Hassan Mabuye
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ikishirikiana na Wizara ya Fedha, imesambaza maafisa wake katika halmashauri 169 kote nchini.

Maafisa hawa wanaotoa mafunzo katika vituo vyote vya makusanyo ya kodi ya ardhi na tozo nyingine kwa kutumia simu ya mkononi ili kuondoa kabisa mfumo wa zamani wa malipo.

Zaidi ya maafisa 170 kutoka makao makuu ya Wizara ya Ardhi, Wizara ya Fedha na kutoka kanda nane za ardhi wameanza kutoa elimu hiyo katika halmashauri na vituo vyote vya makusanyo ya kodi ya ardhi ili kurahisisha ulipaji kodi ya ardhi kwa wananchi kwa kutumia simu zao na kuondoa usumbufu.

Mfumo wa ulipaji kodi ya pango la ardhi kwa njia ya simu ya mkononi ni mfumo wa kielektroniki wa Government electronic Payment Gateway (GePG) katika makusanyo ya kodi ya pango la ardhi ambao utamrahisishia mwananchi kulipia popote walipo kwa kutumia simu zao kwa urahisi zaidi.
Afisa kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bwana Haruna Kiyungi akitoa mafunzo kwa maafisa Ardhi Manispaa ya Nyamagana jinsi ya kutumia Mfumo wa ulipaji kodi ya pango la ardhi kwa njia ya simu ya mkononi/kielektroniki.

Mwananchi yeyote anayemiliki kiwanja au shamba lililopimwa na kupatiwa hati, ataweza kutumia simu yake ya mkononi kujua kiasi cha kodi ya pango la ardhi anachodaiwa na kukulipa kwa kutumia simu yake ya mkononi.

Ili kujua unadaiwa kiasi gani cha kodi ya pango la ardhi kwa kutumia simu ya mkononi bonyeza *152*00# au kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi yaani sms halafu unatuma kwenda namba 15200 na baada hapo unaweza kulipia kwa njia ya Mpesa, Tigo Pesa au kulipia tawi lolote la benki ya NMB na CRDB.

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza rasmi kutumia mfumo huu wa kielektroniki wa GePG katika makusanyo ya kodi ya pango la ardhi pamoja na tozo nyingine zinazotokana na sekta ya ardhi nchini na kuondoa kabisa mfumo wa zamani.

Mfumo huu utamrahisishia mwananchi kulipa kodi ya pango la ardhi popote alipo, ikiwa ni pamoja na kulipia tozo nyingine mbalimbali za sekta ya ardhi. Mmiliki wa kipande cha ardhi ataweza kujua anadaiwa kiasi gani cha kodi ya pango la ardhi na kulipia popote alipo bila kusumbuka kufuata huduma hizo katika vituo vya makusanyo.
Maafisa Ardhi kutoka Manispaa ya Nyamagana, Mwanza wakifuatilia kwa makini jinsi ya kutumia Mfumo wa ulipaji kodi ya pango la ardhi kwa njia ya simu ya mkononi/kielektroniki.

Kwa majaribio ya ukusanyaji kodi ya pango la ardhi kwa kutumia mfumo wa kielektroniki yalifanywa katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani na baada ya mafanikio makubwa kuonekana elimu ikatolewa kwa watendaji wote wa sekta ya ardhi katika Halmashauri zote za mkoa wa Dar es salaam kabla ya zoezi hilo kuhamishiwa mikoani.

Kwa zile huduma nyingine za sekta ya ardhi ambazo zinahusisha malipo kama vile upekuzi katika daftari la msajili (official search), mwananchi atapaswa kutembelea ofisi za Wizara ya ardhi zilizo katika eneo lake na kupatiwa makadirio ya kulipia huduma husika pamoja na namba ya malipo itakayomuwezesha kulipia aidha kwa njia ya benki au simu ya mkononi.

Kwa sasa kikosi kazi kinachotoa mafunzo juu ya matumizi ya mfumo huu kimeshaanza kuelemisha mikoa mingine baada ya kupata mafanikio mazuri katika mkoa wa Dar es Salaam. Lengo kubwa la kutumia mfumo huu ni kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa maduhuli ya serikali pamoja na kurahisisha ulipaji kodi ya pango la ardhi nchini.

Kobe 2500 wakamatwa kwa kumilikiwa kinyume na sheria India

Kobe hutumika kama chakula kwa baadhi ya sehemu za bara la Asia
Image captionKobe hutumika kama chakula kwa baadhi ya sehemu za bara la Asia
Maafisa katika mji wa Tamil Nadu nchini India wamesema wamefanikiwa kukamata zaidi ya kobe 2,500 waliokuwa wanamilikiwa kinyume na sheria.
Kobe hao wamepatikana wakati wa msako mkali katika mji wa Chennai.
Mtu mmoja anashikiliwa na polisi kwa mahojiano.
Kobe hao kwa pamoja wanakadiriwa kuwa na bei ya dola 40,000.
Kuna uhitaji mkubwa wa kobe Asia ya Kaskazini, ambapo hutumika kwa shughuli mbalimbali ikiwemo chakula.

Idadi ya watoto wanaotumiwa kama walipuaji wa kujitolea mhanga yaongezeka Nigeria

Mourners react on July 24, 2017, in the Dalori IDP (Internally Displaced People) camp outside Maiduguri, after a suicide bomb attack that killed fourHaki miliki ya pichaAFP
Image captionThe Boko Haram insurgency has devastated many lives across north-eastern Nigeria
Kumekuwa na ongezeko kwa idadi ya watoto wanaotuimiwa kama washambuliaji wa kujitolea mhanga na wanamgambo wa Boko Haram, kaskazini mashariki mwa Nigeria, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto Unicef, linasema kuwa tayari visa 83 vimeripotiwa mwaka huu, mara nne zaidi ya vile vya mwaka wote wa 2016.
55 kati yao walikuwa ni wasichana walio na umri chini ya miaka 15 na kwenye kisa kimoja, bomu lilifungwa kwa mtot ambaye alikuwa amebewa na msichana mdogo.
Unicef inasema mbinu hii imezua hofu kwa watoto wanaoachiliwa na Boko Haram.
Kulingana na Umoja wa Mataifa, watoto 127 wametumiwa kama walipuaji kaskazini mashariki mwa Nigeria tangu mwaka 2014.
Wanamgambo wa Boko Haram mara kwa mara wamewatumia watoto, na wamewateka mamia ya wasichana wa shule na kuwalazimisha watoto wavulana kujiunga na jeshi lao.

Wahamiaji 20 wakamatwa kwa kusababisha fujo Ufaransa

Whamiaji wakiwa wamejipumzisha barabarani mjini Calais
Image captionWhamiaji wakiwa wamejipumzisha barabarani mjini Calais
Polisi mjini Calais nchini Ufaransa wamekamata watu 20 wanaotuhumiwa kuhusika kwenye fujo kati ya makundi mawili ya wahamiaji.
Takriban wahamiaji 150 kutoka Afghanistan na Eritrea walipigana katika mpaka wa Ufaransa na Uingereza.
Baadhi ya yao walijeruhiwa huku pia wakiharibu magari ya polisi kwa kuyapiga mawe.
Kambi ya wakimbizi ya Calais ilifungwa takriban mwaka mmoja uliopita, lakini ikafunguliwa kutokana na ongezeko la wahamiaji waliokuwa wakitarajia kuingia Uingereza.

Kamanda ya kikosi cha majini cha Marekani kufutwa kazi baada ya manowari kugongwa

Vice Admiral Joseph Aucoin, U.S. 7th Fleet Commander, attends a media briefing on the status of the U.S. Navy destroyer USS Fitzgerald, damaged by colliding with a Philippine-flagged merchant vessel, and the seven missing Fitzgerald crew members, at the U.S. naval base in Yokosuka, south of Tokyo, Japan 18 June 2017.Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionJoseph Aucoin alitarajiwa kustaafu wiki chache zinazokuja
Jeshi la wanamaji la Marekani limesema kuwa litamfuta kazi kamanda Joseph Aucoin wa kikosi cha wanamaji kinachofahamika kama Seventh Fleet, kufuatia visa vya kugongwa kwa manowari za kivita maeneo ya Asia.
Mabaharia 10 bado hawajulikani waliko baada ya manowari ya USS John S McCain kugongana na meli ya kubeba mafuta karibu Singapore siku ya Jumatatu.
Maafisa wa jeshi la wanamaji wanasema kuwa miili ya binadamu imepatikana ndani ya manowari hiyo ambayo kwa sasa imetia nanga katika bandari ya Singapore.
Haki miliki ya picha
Kisa hicho ndicho cha nne ya kugongwa kwa meli mwaka huu.
Kikosi cha Seventh Fleet chenye makao yake huko Yokosuka Japan kina karibu manowari 50 na 70 pamoja na nyambizi.
Joseph Aucoin ambaye amekuwa kamanda tangu mwaka 2015 alikuwa astaafu wiki chache zinazokuja,
Image captio
Kuondolewa kwake ni hatua ya hivi punde kuchukuliwa na maafisa wa jeshi la wanamaji baada ya kisa cha kugongwa kwa manowari ya USS John S McCain. Haijulianai ni lini tangazo rasmi litatolewa.
Manowari ya USS John S McCain ilikuwa mashariki mwa Singapore wakati iligongana na meli ya kubeba mafuta ya Alnic MC mapema siku ya Jumatatu.

Marekani yawekea vikwazo makampuni ya China na Urusi

Kim Jong-unHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKorea inasisitiza kuwa ina haki ya kuwa na mpango wa nyuklia kwa usalama wake
Marekani imetangaza vikwazo kwa kampuni kadha za Urusi na Uchina na watu ambao inawalaumu kwa kusaidia mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.
Hii inajiri baada ya baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa, zikiwemo Urusi na China kupiga kura ya kuiwekea viwazo zaidi Korea Kaskazini.
Wizara ya fedha nchini Marekani ilisema kuwa vikwazo hivyo vitaongeza shinikizo kwa Korea Kaskazini lakini hatua hiyo imeighadhabisha China.
soldiers trainingHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKorea Kaskazini inapinga mazoezi ya pamoja kati ya Korea Kusini na Marekani
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani Rex Tilleron, wakati huo huo ameipongeza Korea Kaskazini kwa kujizuia siku za hivi karibuni.
"Hatujashuhudia urushaji wa makombora na vitendo vya uchokozi kutoka Korea Kaskazini tangu azimio la baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa lianze kutekelezwa," alisema.
Wizara ya fedha itaendelea kuongeza shinikizo kwa Korea Kaskazini kwa kuenga wale wanaosaidia kuendelea kwa mipango ya nyuklia na ya makombora ya masafa marefu.
Haki miliki ya ES
Image caption
Hatua hiyo inamaanisha kuwa watu nchini Marekani na kampuni za Marekani haziruhusiwi kufanya biashara na kampuni zinazosaidia programu za Korea Kaskazini.
China ilijibu mara moja kwa kutoa wito kwa Marekani ikitaka irekebishe makosa yake ya kuadhibu makampuni ya China.

Marekani yawekea vikwazo makampuni ya China na Urusi

Kim Jong-unHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKorea inasisitiza kuwa ina haki ya kuwa na mpango wa nyuklia kwa usalama wake
Marekani imetangaza vikwazo kwa kampuni kadha za Urusi na Uchina na watu ambao inawalaumu kwa kusaidia mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.
Hii inajiri baada ya baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa, zikiwemo Urusi na China kupiga kura ya kuiwekea viwazo zaidi Korea Kaskazini.
Wizara ya fedha nchini Marekani ilisema kuwa vikwazo hivyo vitaongeza shinikizo kwa Korea Kaskazini lakini hatua hiyo imeighadhabisha China.
soldiers trainingHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKorea Kaskazini inapinga mazoezi ya pamoja kati ya Korea Kusini na Marekani
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani Rex Tilleron, wakati huo huo ameipongeza Korea Kaskazini kwa kujizuia siku za hivi karibuni.
"Hatujashuhudia urushaji wa makombora na vitendo vya uchokozi kutoka Korea Kaskazini tangu azimio la baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa lianze kutekelezwa," alisema.
Wizara ya fedha itaendelea kuongeza shinikizo kwa Korea Kaskazini kwa kuenga wale wanaosaidia kuendelea kwa mipango ya nyuklia na ya makombora ya masafa marefu.
soldiers trainingHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKorea Kusini inasema kuwa mazoezi hayo ni ya kujikinga
Hatua hiyo inamaanisha kuwa watu nchini Marekani na kampuni za Marekani haziruhusiwi kufanya biashara na kampuni zinazosaidia programu za Korea Kaskazini.
China ilijibu mara moja kwa kutoa wito kwa Marekani ikitaka irekebishe makosa yake ya kuadhibu makampuni ya China.

Kikwete ajipanga kuanzisha kiwanda


Rais wa Awamu ya nne, Jakaya Kikwete (kulia)

Rais wa Awamu ya nne, Jakaya Kikwete (kulia) akiangalia mahindi ya njano yanayoendelea kuvunwa shambani kwake Msoga,  Chalinze mkoani Pwani. Kikwete amesema ataitumia nafaka hiyo kwa virutubisho na malisho ya ng’ombe wake anaowafuga kijijini hapo. Picha na Julieth Ngarabali 
Chalinze. Rais wa Awamu ya nne, Jakaya Kikwete amesema yupo mbioni kufungua kiwanda cha usindikaji wa maziwa na siagi kwa sababu sasa anapata lita zaidi ya  200  za maziwa kila siku.
Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Msoga jana, Kikwete alisema mpango alionao ni kuanzisha kiwanda cha kusindika maziwa na siagi kwa sababu ana uhakika atakimudu.
Alisema anaweza kufungua kiwanda hicho kwa sababu kwa sasa ana ng’ombe zaidi ya 400 na  mpango wake ni kuongeza wengine wa maziwa.
“Inawezekana kabisa kwa sababu ukitaka kufungua kiwanda kama hicho unatakiwa kuhakikisha kwamba una ng’ombe wa kutosha, malisho  na  uhakika wa kuwapatia matibabu,’’ alisema
“Nimeanza kilimo na ufugaji  tangu  miaka ya 1988/1989 na ndiyo maana namudu kusimamia na kupata faida,” alisema  Kikwete.
Alisema watu wasipende kusubiri  muda wa kustaafu ndiyo waanze kujishughulisha na kilimo au ufugaji kwani kazi hizo zina changamoto zake ambazo kama mtu hakuzizoea tangu awali anaweza kukwama.
Alisema msimu huu amelima ekari 30 za mahindi ya njano na jana  alivuna ekari nne tu za kwanza.
Mstaafu huyo alifafanua kuwa aliamua kulima aina hiyo ya mahindi ili aweze kupata malisho na virutubisho vya mifugo yake kwani nafaka hizo zina nguvu zaidi ya mahindi ya kawaida.
Alipoulizwa kuhusu hali ya kisiasa hapa nchini na uchaguzi mkuu wa Kenya, Kikwete alisema ‘no comment’ (sina cha kusema) kwani yeye ni mkulima na mfugaji na mambo mengine alishawaachia wengine.
Alisema kuwa hata akiwa nyumbani kwake ametulia hapendi kuzungumzia ya wengine waliopo sasa kwani kila nyakati na watu wake na staili yake.
“Jamani mimi niulizeni mambo ya kilimo na ufugaji tu, masuala mengine sijui ya nchi au hata hili la uchaguzi wa Kenya msiniulize jamani, mimi kwa sasa ni mstaafu, mambo ya serikali wapo wenyewe, mimi nilishamaliza kazi yangu, kama kushauri au kufanya nilishafanya niliyoweza na nikawaachia wengine,”alisema Kikwete ambaye aliongoza nchi kwa vipindi viwili vya miaka kumi kuanzia mwaka 2005 mpaka 2015 .

Lissu anyimwa dhamana


Mwanasheria wa Chadema na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amenyimwa dhamana baada ya kukamatwa leo kwa tuhuma za kumkashifu Rais John  Magufuli na uchochezi.
Akizungumza na Mwananchi leo  mwanasheria wake Faraji Mangula amesema kwamba kesho Lissu atapandishwa mahakamani.
Amesema Polisi wamedai kwamba amemkashifu Rais a wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari  kwenye hoteli ya Protea.
‘’Polisi wamemnyima dhamana wamesema wanafanya utaratibu wakumfikisha mahakamani’’amesema.

UTATA: RC Arusha, Kilimanjaro ‘lugha gongana’


Arusha. Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amezikabidhi familia tatu za watoto walionusurika katika ajali ya Lucky Vincent Sh23.2 milioni zilizokusanywa kwa ajili ya rambirambi baada ya ajali hiyo iliyotokea Mei 6, mwaka huu wilayani Karatu kuua wanafunzi 32, walimu wawili na dereva.
Akizungumza ofisini kwake jana na familia hizo, Gambo alisema Serikali na wadau wamechangia fedha ambazo zilitumika katika shughuli nzima za mazishi ya marehemu hao na kiasi kilichobaki zinakabidhiwa kwa familia hizo ili  kiwasaidie.
Hata hivyo, wakati Gambo akisema hayo baada ya kutoa fedha hizo, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira ambaye alimwakilisha Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan kuwapokea wanafunzi hao waliporejea kutoka kwenye matibabu huko Marekani Agosti 18, aliagiza Serikali ya Mkoa wa Arusha kutoa Sh20 milioni ambazo ni sehemu ya michango hiyo kuchangia mfuko wa elimu wa Stemm.
Lakini jana Gambo alisema, “Kimsingi napenda kumshukuru Mungu kwa kuwasaidia watoto wetu hawa na wadau wengine waliowezesha kupata matibabu nchini Marekani na wamerudi salama, katika fedha tulizokusanya tumeamua kila familia kati ya hizi  tatu tuzikabidhi  Sh7,750,000 kwa ajili ya matumizi yao.”
Alipoulizwa kuhusu kuwapa wahusika fedha hizo moja kwa moja ilhali maagizo ya Makamu wa Rais yalitaka zielekezwe kwenye mfuko wa elimu unaolenga kuwasaidia alisema Serikali huwa inafanya kazi kwa maandishi na ofisi yake haikuwa imepokea maagizo yoyote. Alisisitiza kuwa uamuzi wa kuwakabidhi umeridhiwa na uongozi wa mkoa huo.
Alisema yeye ndiye aliyemuomba Mghwira akawapokee watoto hao kwa kuwa alikuwa nje ya Arusha kwa majukumu mengine. Alipoulizwa kuhusu hotuba aliyoisoma kama ilikuwa ya Makamu wa Rais au mkuu wa mkoa mwenzake alisema mwenye majibu sahihi ni Mghwira.
Hata hivyo, Mghwira alipotafutwa jana kufafanua utata huo alijibu kuwa alikuwa kwenye kikao muhimu.
Baada ya kukabidhiwa fedha hizo, wazazi wa Doreen Mshana, Wilson Tarimo na Sadia Awadh walizishukuru serikali za Tanzania na Marekani taasisi za Stemm, Samaritan’s Purse na wadau wengine waliofanikisha matibabu ya watoto wao.
“Sisi wazazi tunawashukuru sana kwa msaada mkubwa mliotufanyia na kuwawezesha watoto wetu kupata matibabu. Mungu awabariki sana kwa sababu sisi wenyewe tusingeweza,” alisema mmoja wa wazazi hao, Neema Matemba.
Mitihani ya darasa la saba
Mzazi wa Doreen, Elibariki Mshana alimwomba Gambo aiingilie kati suala la watoto wao kufanya mitihani kwani dalili zinaonyesha kuwa uongozi wa shule hauko tayari kuwaruhusu kutahiniwa kutokana na kutokuwapo darasani kwa muda mrefu.
“Wazazi na wanafunzi wetu tupo tayari ili wafanye mitihani mwezi ujao lakini naona kama uongozi wa shule unasita kuwaruhusu, tusingependa warudie mwaka tunaamini watafanya vizuri mitihani yao tusiwekewe kikwazo,” alisema Mshana.
Gambo alisema iwapo wanafunzi hao wapo tayari kufanya mitihani yao na wazazi wameridhia haoni sababu ya kuzuiwa na kumwagiza ofisa elimu wa mkoa kufuatilia suala hilo na kulipatia majibu mapema.