Wednesday, August 23

Marekani yawekea vikwazo makampuni ya China na Urusi

Kim Jong-unHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKorea inasisitiza kuwa ina haki ya kuwa na mpango wa nyuklia kwa usalama wake
Marekani imetangaza vikwazo kwa kampuni kadha za Urusi na Uchina na watu ambao inawalaumu kwa kusaidia mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.
Hii inajiri baada ya baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa, zikiwemo Urusi na China kupiga kura ya kuiwekea viwazo zaidi Korea Kaskazini.
Wizara ya fedha nchini Marekani ilisema kuwa vikwazo hivyo vitaongeza shinikizo kwa Korea Kaskazini lakini hatua hiyo imeighadhabisha China.
soldiers trainingHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKorea Kaskazini inapinga mazoezi ya pamoja kati ya Korea Kusini na Marekani
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani Rex Tilleron, wakati huo huo ameipongeza Korea Kaskazini kwa kujizuia siku za hivi karibuni.
"Hatujashuhudia urushaji wa makombora na vitendo vya uchokozi kutoka Korea Kaskazini tangu azimio la baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa lianze kutekelezwa," alisema.
Wizara ya fedha itaendelea kuongeza shinikizo kwa Korea Kaskazini kwa kuenga wale wanaosaidia kuendelea kwa mipango ya nyuklia na ya makombora ya masafa marefu.
soldiers trainingHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKorea Kusini inasema kuwa mazoezi hayo ni ya kujikinga
Hatua hiyo inamaanisha kuwa watu nchini Marekani na kampuni za Marekani haziruhusiwi kufanya biashara na kampuni zinazosaidia programu za Korea Kaskazini.
China ilijibu mara moja kwa kutoa wito kwa Marekani ikitaka irekebishe makosa yake ya kuadhibu makampuni ya China.

No comments:

Post a Comment