Thursday, November 23

Polisi wavamia wahamiaji Papua New Guinea

Mamlaka zikiwaondosha wanaoomba uhamiaji Papua New GuineaHaki miliki ya pichaAFP PHOTO / GETUP
Image captionMaafisa wa Papua New Guinea walikuwa wamewapatia wahamiaji muda wa kuondoka.
Polisi wa Papua New Guinea (PNG) wameingia katika kituo cha mahabusu cha wahamiaji kilichokuwa kinamilikiwa na Australian kwa azma ya kuwaondosha wanaoomba uhamiaji waliosalia, imethibitisha serikali ya Australia.
Mamia ya wanaume wamekataa kuondoka kwenye kituo hicho kilichopo katika kisiwa cha Manustangu kilipofungwa tarehe 31 Oktoba, wakielezea hofu ya usalama wao.
Alhamisi, wanaume waliokuwa katika kituo hicho walisema polisi wa PNG walikuwa wamewapatia saa moja wawe wameondoka.
Australia imesema kuwa operesheni hiyo inaendeshwa na Papua New Guine- PNG.
Chini ya sera tata, Australia iliwashikilia watu wanaoomba uhamiaji wanaowasili kwa boti kwenye kambi katika visiwa cha Manus na Nauru, ambalo ni taifa dogo leneo la Pacific.
Image copyrightABDUL AZIZ ADAM
Uharibifu wa vifaa katika kituo cha wahamiajiHaki miliki ya pichaABDUL AZIZ ADAM
Image captionMahabusu wa zamani anasema maafisa wameharibu vifaa kwatika kito cha kuwahifadhi wahamiaji
Australia ilifunga kituo hicho cha kisiwa cha Manus baada ya mahakama ya PNG kuamua kuwa kilikuwa ni kinyume cha sheria, na kuwataka wanaoomba uhamiaji kuhamia kwenye vituo vingine vya wanaoomba uhamiaji vilivyopo kwenye maeneo mengine ya kisiwa hicho.
Waziri mkuu wa Australia Malcolm Turnbull alisema kuwa taifa lake ''halitashinikizwa " kuwakubali wanaume hao wahamiaji, akirejelea kuwa sera ya muda mrefu ya kuwashikilia itachochea biashara haramu ya binadamu.
" Wanapaswa kuheshimu sheria na mamlaka za kisheria za Papua New Guinea,"Alisema waziri mkuu wa Australia Bwana Turnbull.
Mmoja wa wakimbizi hao, Abdul Aziz Adam, alisema kwua watu wapatao 420 wanaoomba uhamiaji walibakia kwenye kituo hicho Alhamis Thursday, na walikuwa watulivu.
Watu hao walikataa kuondoka kwasababu wanahofia kuwa wanaweza kushambuliwa na jamii za watu waishio kwenye kisiwa hicho.
Makundi ya kutete haki za binadamu yansema wahamiaji hao wamewahi kushambuliwa awali.

SAFARI YA KAFULILA, CHADEMA – NCCR – CHADEMA – ‘CCM’




MBUNGE wa zamani wa Kigoma Kusini, David Kafulila, ametengeneza historia nyingine kisiasa, hasa baada ya kutangaza kuhama Chadema.
Hatua hiyo inatajwa kama historia ya aina yake kwa mwanasiasa huyo, ambaye ametumikia vyama viwili tofauti katika kipindi cha miaka 10, huku akitarajiwa wakati wowote kujiunga na chama kingine hivi karibuni.
Kafulila alitangaza uamuzi wa kujivua uanachama wa Chadema jana katika taarifa yake, huku akidai kwamba hana imani tena na upinzani katika kupambana na ufisadi.
Hii ni mara ya pili kwa Kafulila kutoka Chadema baada ya mwaka 2009 alipoondoka na kujiunga na NCCR-Mageuzi.
Hatua ya mwanasiasa huyo kijana, imekuja siku moja baada ya juzi Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), kuridhia kupokewa kwa waliokuwa wanachama wa Chadema; aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrance Masha na Mwenyekiti wa Bavicha, Patrobas Katambi.
Katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari, Kafulila, alidai kwamba kwa sasa bado anatafakari na hivi karibuni atatangaza jukwaa jipya, akimaanisha chama atakachohamia ili kuendeleza harakati zake dhidi ya ufisadi.
Akielezea sababu za kuhama Chadema ikiwa ni miezi 11 tu tangu ahamie akitokea NCCR-Mageuzi, alisema ni upinzani kukosa ajenda ya ufisadi.
Kafulila, alisema hiyo inatokana na Rais Dk. John Magufuli kushughulikia kwa vitendo ajenda ya ufisadi, hasa baada ya watuhumiwa na wahusika wa rushwa kubwa kufikishwa mahakamani.
“Nikiwa mmoja wa wanasiasa vijana, nilibahatika kutumikia Bunge la 10, siku zote nimejipambanua na kujitoa mhanga kupambana na ufisadi kupitia jukwaa la Bunge, vyama vya siasa na shughuli mbalimbali za kijamii kwa ujumla.
“Hata hivyo, katika siku za hivi karibuni na hasa tangu harakati za uchaguzi mwaka 2015, vyama vya upinzani nchini vinaonekana kupigwa ganzi na kupooza katika juhudi zake za kupambana na ufisadi.
“Tangu Rais Magufuli achaguliwe na kukabidhiwa jukumu la kuongoza nchi, vita ya miaka mingi dhidi ya ufisadi imechukua sura mpya.
“Ghafla ufisadi siyo tena ajenda kuu ya upinzani nchini kwa sababu ni wazi kuwa upinzani siyo tena jukwaa la kuendesha vita dhidi ya ufisadi,” alisema Kafulila katika taarifa yake.
Aidha, Kafulila alisema matokeo ya tafiti za hivi karibuni zilizofanywa na mashirika huru ya ndani na nje ya nchi zinaonyesha kiwango cha rushwa nchini kimeporomoka.

TAARIFA ZA KUZUIWA NA MKEWE KUJIUNGA CCM
Hata hivyo, MTANZANIA ilipomtafuta Kafulila, ili kujua uwepo wa taarifa ya kushindwa kujiunga na CCM juzi akidaiwa kuzuiwa na mkewe Jesca Kishoa ambaye ni mbunge wa viti maalumu Chadema, alizikanusha.
“Hakuna mwenye uhusiano wa mapenzi na siasa, ni tofauti, nilikuwa NCCR akiwa Chadema. Kwahiyo hakuna uhusiano wowote ule, hii ni nafasi yangu,” alisema.
Alipoulizwa wakati akiwa Chadema walikuwa pamoja na mkewe, alisema: “Siasa ni kile unachoamini, yaani unaamini katika nini… Dk. Slaa alikuwa Chadema mke wake alikuwa CCM, nini tatizo?
“Na alikuwa anaonyesha kupambana na rushwa kuliko mwanasiasa yeyote. Na ukisema alikuwa anamwibia siri mumewe si kweli, yaani diwani anaweza akajua siri za chama kikubwa kama CCM? Hata kwa akili ya kawaida tu diwani anaweza akajua siri za ngazi ya taifa?”
Alipoulizwa kuhusu hatima ya mke wake kama naye ataamua kuondoka Chadema au la, alisema atafutwe mwenyewe kwani naye ana msimamo wake wa kisiasa.

ALIVYOKUWA CHADEMA
Kafulila ambaye aliwahi kuwa Ofisa Habari wa Chadema kabla hajatimkia NCCR-Mageuzi mwaka 2009, baada ya kuhama mwaka huo, aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, alidai kuondoka kwake hakukuwa na athari yoyote kwani alikuwa sisimizi tu ndani ya chama hicho.
Hatua hiyo aliichukua baada ya kuwatuhumu Mwenyekiti Freeman Mbowe na Dk. Slaa kuwa wanaendesha chama hicho kibabe na kwamba katika uongozi wao mbovu, wamekuwa na matumizi mabaya ya fedha za ruzuku.
Kutokana na hali hiyo, kulikuwa na tetesi kwamba kama angeendelea kuwa ndani ya Chadema, basi jina lake lisingepitishwa kwani alitaka kugombea ubunge katika Jimbo la Kigoma Kusini, mwaka 2010.
Kwa mujibu wa Kafulila kwa wakati huo, alidai kwamba chuki ya Mbowe na Dk. Slaa ndiyo ilimwondoa Chadema baada ya kuhoji matumizi ya fedha za chama, zikiwamo Sh milioni 35 za ruzuku ambazo wakati huo haikujulikana zilipo.

NCCR-MAGEUZI
Akiwa katika chama cha NCCR-Mageuzi, Kafulila alifanikiwa kushinda ubunge Jimbo la Kigoma Kusini hadi mwaka 2015.
Katika harakati zake ilidaiwa Kafulila na wenzake walijaribu kupanga mkakati kumpindua Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia wakimtaka kujieleza kuhusu kukidhoofisha chama na kuwa kibaraka wa CCM.
Hata hivyo, jaribio hilo lilifeli na kuishia kuvuliwa wadhifa wa Katibu Mwenezi wa chama hicho, huku akifukuzwa uanachama na alikimbilia mahakamani kupinga uamuzi huo.

MAPAMBANO BUNGENI
Akiwa bungeni, Kafulila alijizolea umaarufu, hasa baada ya kuibua sakata la uchotwaji wa fedha kwenye akaunti maalumu ya Tegeta Escrow, lililosababisha mvutano mkali baina yake na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema.
Werema alimfananisha Kafulila na ‘tumbili’, akidai kuwa hakuwa anajua anachokisema.
Katika majibizano hayo bungeni, yaliyosababisha Bunge kusimama kwa muda, Kafulila alijibu mapigo kwa kumwita Jaji Werema ‘mwizi’, huku akitaka uchunguzi ufanyike ili ifahamike nani ni tumbili na nani ni mwizi.
Aidha, Kafulila aliwalipua kwa kuwataja kwa majina baadhi ya viongozi wa dini na Serikali, akidai walipokea mgawo wa fedha hizo za Escrow.

AREJA CHADEMA
Desemba mwaka jana, Kafulila alitangaza kuhama NCCR-Mageuzi na kuhamia Chadema kwa madai kuwa chama hicho hakina mwelekeo wa kuleta mabadiliko na kwamba anahamia katika chama kinachojipambanua kimkakati na mipango kuleta mabadiliko ya kweli.
Hata hivyo, Kafulila alidaiwa kuhama NCCR-Mageuzi baada ya kushindwa kutetea ubunge wake wa Kigoma Kasini mwaka 2015 licha ya kupambana mahakamani kudai haki yake.
Juzi Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (Bavicha), Patrobas Katambi na Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani, Lawrance Masha walitangaza kujiunga na CCM.
Kutoka ACT-Wazalendo waliojunga na CCM ni aliyekuwa mshauri wa chama hicho ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo, aliyekuwa Katibu Mkuu Samson Mwigamba, Mshauri wa Sheria, Albert Msando na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Edna Sunga.

MARUFUKU KUMZUNGUMZIA LISSU KWENYE KAMPENI-MWIGULU


WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba, amevionya vyama vya upinzani kuacha kuzungumzia suala la shambulio la Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), katika kampeni za udiwani nchini.
Kauli hiyo ameitoa jana wakati wa kampeni za kumnadi Mgombea Udiwani wa CCM wa Kata ya Chanikanguo, Cypria Mpetula, katika mkutano wa kampeni huku akivitaka vyama hivyo kunadi sera za wagombea wao badala ya shambulio la Lissu.
“Mimi nashangaa sana badala ya kunadi sera zao wamekazana kutangaza shambulio la Lissu, hivi shambulio la Lisssu linahusiana vipi na Kata ya Chanikangu.
“Haiwezekani kila siku wanashindwa kunadi sera  zao, labda kuna jambo fulani wao walitarajia lifanyike ili wailaumu Serikali wanavyojifanya wana uchungu sana kuliko  hata mimi ambaye Lissu ni ndugu yangu tunatoka wote Singida,” alisema Mwigulu.
Katika hatua nyingine, Mwigulu ameliomba Jeshi la Polisi Wilaya ya Masasi kulipitia upya jalada la kesi la mgombea wa udiwani Kata ya Chanikanguo kwa tiketi ya Chadema na kuchunguza  upya kwa kuwa kesi za jinai huwa hazina ukomo.
Alisema mgombea huyo anatuhumiwa kuiba mabati 20,000 katika Halmashauri Mji wa Masasi alipokuwa Lindi kwenye kampuni moja ya ulinzi na magunia manne ya korosho alipokuwa mjumbe wa bodi ambazo baadaye alizirudisha baada ya kubanwa.
“Jeshi la Polisi pitieni upya kesi yake na kuichunguza juu tuhuma zinazomkabili mgombea huyo, mashahidi wapo haiwezekani tukawa na mgombea mwenye sifa mbaya ya wizi halafu aje kutuongozea kata yetu, kama ameshindwa kulinda mali za halmashauri ya mji alipokuwa ni askari, atawezaje kuwa na uaminifu wa kulinda mali za kata akiwa diwani?
“Ninaomba wale pia wanaoshiriki katika kunadi mambo hayo wachunguzwe pia,” alisema Mwigulu.
Kwa upande wake mgombea udiwani Kata ya Chanikanguo, Cypria Mpetula, aliwaomba wananchi wamchague kwa kuwa anaweza kuwaletea maendeleo kwani anao uzoefu wa uongozi kwa muda mrefu kama katibu wa kata hiyo.

Ufaransa yataka Libya kujadiliwa na UN

Wahamiaji kutoka AfrikaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWahamiaji kutoka Afrika
Ufaransa imetoa wito wa kufanyika mkutano katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kujadili vitendo vibaya wanavyofanyiwa Wahamiaji nchini Libya.
Hatua hiyo imekuja baada ya taarifa kutoka nchini Libya kusema kuwa Wahamiaji wa Kiafrika wamekuwa wakiuzwa kama watumwa.
Baada ya mkutano wake na Kiongozi wa Umoja wa Afrika, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amekuelezea kuuzwa huko kama uhalifu dhidi ya ubinadamu na kuongeza kuwa hatua zaidi zinahitajika kuchukuliwa kuvunja mtandao wa watu wanaohusika na biashara haramu ya binadamu.
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian amesema vikwazo vya kimataifa vinapaswa kuwekwa iwapo mamlaka za Libya hazitachukua hatua, kupiga marufuku vitendo hivyo.

Kujiuzulu kwa Mugabe: Kimya kirefu cha rais Zuma chawashangaza wengi

Bwana Robert Mugabe wa Zimbabwe na rafikiye rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini
Image captionBwana Robert Mugabe wa Zimbabwe na rafikiye rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini
Kimya kirefu cha rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma pamoja na chama chake tawala cha ANC kufuatia kujiuzulu kwa Robert Mugabe kinashangaza.
Kinaonyesha ushawishi wa kisaikolojia aliyokuwa nao kwao na walishangazwa sana na hatua aliyochukua.
Kile afisi ya rais Zuma ilichosema ni kwamba hatoweza tena kuelekea nchini Zimbabwe kama alivyokuwa amepanga ili kupatanisha kbal ya rais Mugabe kutangaza kujiuzulu.
Ziara hiyo sasa imeahirishwa hadi tyangazo jingine , taarifa ilisema.
Lakini badala yake chma cha upinzani nchini Afrika Kusini DA kilijibu na hivyobasi kuungwa mkono na raia weusi pamoja na wazungu kiliposema:
Huu ni ushindi wa raia wa Zimbabwe ambao wametaabika chini ya uongozi wa Mugabe .Habari ya bwana Mugabe sio geni na kwamba inaendelea katika bara la Afrika.Mtu aliyekuwa shujaa wa taifa lake , Mugabe alisababisha migawanyiko, ukosefu wa udhabiti na kuharibika kwa uchumi wakati alipobadilika kutoka kuwa mpiganiaji wa uhuru hadi kuwa dikteta.Hilo sio tu kwa Mugabe bali hata Zanu -PF chama ambacho amekitawala kwa kutumia nguvu kwa kuchukua mamlaka tangu taifa hilo lijipatie Uhuru.Chama cha ANC kinaonyesha ishara kama zile za Zanu-PF, kimekumbwa na ufisadi mkubwa na ghasia huku pande pinzani zikipigania madaraka katika serikali kwa lengo la kujitajirisha badala ya kuwahudumia wananchi.Baada ya kuchukua madaraka miaka 23 kutoka kwa wazungu ,ANC sasa kinakabiliwa na changamoto ya kujiimarisha au tishio la kuangamiza uchumi wa Afrika kusini kama Zanu-Pf kilivyofanya kwa miaka 37.

Raia wa Uingereza aliyeiomba mahakama imfunge''

Bradley Grimes
Image captionTabia ya Bradley ya hali ya kutopenda maisha ya kijamii ilimzuwia ''kuzurura" karibu na maeneo ya biashara
Baada ya kupigwa marufuku kuomba na kulala ovyo ovyo kwenye veranda za maduka katika mji wa Middlesbrough, Bradley Grimes alimuomba jaji wa mahakama ammpeleke gerezani kuliko kumuacha bila makazi .
Itakuwa na athari gani? " Kile walichokifanya ni kunifanya nisipende kuishi katika jamii kujaribu kunizuwia nisiwe omba omba.
Lakini lazima niombe ili kuweza kuishi," Bradley Grimes alimueleza mwandishi wa BBC.
Alikosa makazi ya kuishi baada ya kuondoka kwenye mfumo wa misaada ya jamii akiwa na umri wa miaka 17.
Bradley Grimes mwenye tatizo la kigugumizi na ''akili ya kitoto'' hakuweza kupata kazi na mara kwa mara amekuwa omba omba- akiwaomba wasafiri chakula na pesa kando ya mtaa wenye shughuli nyingi.
Bradley Grimes
Image captionHapa ndipo Bradley anasema hulala mara kwa mara, kando kidogo ya bara bara yenye shughuli nyingi
Lakini hii ilimfanya jaji katika mahakama ya Middlesbrough kumuamrisha kuacha tabia hiyo
Amri hiyo iliambatana na amri ya kumzuwia " kuzurura" nje ya majumba ya biashara.
Bradley anasema amri hiyo ilimzuwia "kukaa nje ya duka " na kulala kwenye bveranda za maduka ambako alikuwa akipata joto, na hilo lilimfanya kuendelea kukamatwa na maafisa wa usalama.
" mitambo ya kamera ya CCTV inachukua picha na kuituma moja kwa moja kwa polisi au walinzi wa mitaa. Polisi wakija, unakamatwa ," alieleza Bradley, ambaye sasa ana umri wa miaka 23.
Anasema kilichomfanya maafisa wa usalama ni kukaamkabala ni kituo cha basi.
Bradley Grimes akiwa kwenye kituo cha mabasi
Image captionBradley anasema kuwa wakati mmoja alikamatwa alipokuwa ameketi mkabala na kituo cha basi
"Nilifika kwenye kituo ambako walinifunga mara moja ama mara mbili kwa siku, katika kipindi cha miezi michacheg
"Nilikuwa nafungwa zaidi nyakati za mwishoni mwa juma.
"Siwezi hata kukaa kwenye kiti cha umma bila kutiwa nguvun. Inabidi nishinde nikizurura ."Kutokana na kuchoshwa na hali hii, aliamua kuomba msaada usio wa kawaida at his situation, he decided to seek .
Alipokuwa mahakamani, akishtakiwa kwa kukiuka hukumu ya kifungo cha nyumbani cha miezi minne- kosa mabalo alikiri kulifanya - alimuomba jaji kumuweka jela,.

Mashirika yasiokuwa ya kiserikali Urusi yaandamwa lakini hayajasalimu amri

Tangu mwaka 2012, mashirika yasiyo ya kiserikali ya Kirusi na yanayofadhiliwa kimataifa yamelazimika kujiandikisha kama "mawakala wa kigeni." Licha ya unyanyapaa huu, wengi wao wanajikakamua.

Karte Inguschetien Englisch
Miaka mitano baadaye, DW inalitazama jambo hili kwa makini.
Kwa Marina Koltsova na wenzake, jimbo la Chechnya ni eneo lolote lisiloendeka, eneo tupu kwenye ramani. "Kama jambo la msingi, haturuhusiwi kufanya semina katika kanda ya kaskazini mwa Caucasus, kwa sababu tu tunakabiliwa na unyanyapaa huo," Koltsova, mwanasheria wa shirika la masuala ya haki za binadamu maarufu "Memorial," jijini Moscow aliiambia DW.
"Taasisi za kiserikali katika ngazi zote zimekuwa zinatuambia wazi kwamba tumewekwa kama mawakala wa kigeni - hiyo ina maana wapelelezi - na kwamba hawawezi kushirikiana nasi. Mamlaka zimejulishwa kwa mdomo au hata kwa maandishi," alisema.
Sio tu wanaharakati wa haki za binadamu
Kizuizi hiki ni matokeo ya moja kwa moja ya sheria ambayo ilianza kutumika miaka mitano iliyopita: mnamo 21 Novemba 2012.
Chini ya sheria hiyo, mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yanafanya kazi kisiasa na kupokea fedha kutoka ng'ambo yanatakiwa kujiandikisha kama "mawakala wa kigeni."
Kwa kuongeza, wanatakiwa kufanya hayo hadharani, kwenye tovuti zao, kwa mfano, na lazima wafafanue vyanzo vya fedha zao haraka.
Mashirika ya haki za kibinadamu yanaathirika zaidi, lakini pia mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yanafanya kampeni kwa ajili ya mazingira au masuala ya huduma za afya.
Russland Moskau-Büro der NGO Memorial (Getty Images/AFP/Kudryavtsev)
Shirika lisilo la kiserikali la ´Memorial´ liliorodheshwa kwenye regista ya ´mawalaka wa kigeni´ bila ya idhini
Sheria ya "mawakala wa kigeni" ilikuwa moja ya mfululizo wa hatua za kuzuizi ambazo zilianzishwa na serikali ya Kirusi kwa kukabiliana na harakati ya kupinga vuguvugu la upinzani la Kremlin ambalo lilizuka katika kipindi kati ya  uchaguzi wa bunge na wa rais wakati wa mwaka 2011/12.
Machoni mwa viongozi wa Kirusi, mashirika yasiyo ya kiserikali ni vyombo vinavyotumiwa na serikali za magharibi kutaka kubadilisha uongozi nchini humo.
Rasmi, Urusi iliteteta hatua yake hii kwa kugusia juu ya sheria ya Marekani  juu ya usajili wa mashirika ya nje  inayovitaka vyombo vya nje kutoa taarifa za shughuli zao kwa umma.
Wataalamu, hata hivyo, wanazingatia kulinganisha moja kwa moja kati ya vipande viwili vya sheria kuwa na matatizo, kwa sababu nchini Urusi neno "wakala wa kigeni" limehusishwa na ujasusi tangu zama za kisovieti.
Kuharibiwa muonekano ni tatizo kubwa zaidi, alisema Marina Koltsova wa taasisi ya "Memorial," ambayo inafanya kazi kukuza kumbukumbu ya ukandamizaji wa kisiasa katika Muungano wa Sovieti.
Kwa mashirika mengi yasiyokuwa ya kiserikali, sheria hiyo ni kikwazo kikubwa na, hivyo walikataa kujiorodhesha kwa hiari katika orodha ya "wakala wa kigeni" ya Wizara ya Sheria.
Walipata msaada kutoka Baraza la Ulaya, Umoja wa Ulaya na serikali za Magharibi.
Na kulikuwa na upinzani kutoka ndani ya Urusi, pia, kwa mfano kutoka Baraza la Rais la Mashirika ya Kiraia na Haki za Binadamu. Lakini hakuna kilichosaidia.
Hatimaye, Wizara ya Sheria ilifanya jukumu thabiti na kuziorodhesha mashirika yasiokuwa ya kiserikali kwenye rejista ya "mawakala wa kigeni" bila idhini yao.
Miaka mitano sasa, tathmini ya jumla ni mchanganyiko. Baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali, kama Helsinki iliyoko jijini Moscow, kwa mfano, walijiondolea kabisa msaada wa nje ya nchi na wameendelea kuwepo.
Wengine wengi waliwasilisha kesi za kisheria katika mahakama za Kirusi ambazo hazikufaulu - ikiwa ni pamoja na "Memorial", akikumbuka Marina Koltsova: "Mahakama zinaamini kwamba kufanya maonyesho au meza ya mzunguko inapeleka shughuli za kisiasa," alisema.
Memorial ni miongoni mwa mashirika 60 yasiyokuwa ya serikali ambayo yamewasilisha mashtaka na mahakama ya haki za binadamu ya Ulaya huko Strasbourg. Uamuzi unatarajiwa mwishoni mwa mwaka 2018.

Wadukuzi waiba habari za mamilioni ya wateja wa Uber

Uber ilifichua kwamba wadukuzi waliiba habari za mamilioni ya wateja kutoka kwa sava za kampuni hiyo ya kiteknolojia.
Kampuni ya kiteknolojia ya kuwaunganisha wasafiri na madereva wa magari, Uber, ilifichua Jumanne kwamba wahalifu wa kimitandao waliingia kwenye sava zake na kuiba nyaraka zenye ripoti kuhusu takriban wateja milioni 57.
Licha ya hudukuzi huo kutokea mwaka uliopita, maafisa wakuu wa kampuni hiyo hawakutoa habari hizo hadi sasa.
Afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo, Dara Khosrowsawi, ambaye alichukua usukani mwezi Agosti, alifichua yaliyojiri kupitia taarifa.
Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, afisa huyo alisema habari zilizoibwa ni pamoja na majina ya wateja, anwani zao za barua pepe, nambari za simu na habari kuhusu leseni za kuendesha magari.
Aidha Khosroshawi alifichua kwamba Uber iliwalipa wahalifu hao dola elfu mia moja, hili kuharibu na kutozitumia nyaraka hizo.
Tayari kampuni huiyo imeshutumiwa vikali na wadau, ambao wanahoji kama lilikuwa jambo la busara kuwalipa wahalifu hao wa kimitandao.
Hata hivyo, afisa huyo mkuu amejiondoa kwa lawama kwa kusema kuwa hayo yalitendeka wakati wa wa uongozi wa afisa mkuu mtendaji aliyemtangulia, Travis Kalanick.
Licha ya kupanua biashara yake kwa kasi mno katika kipindi cha miaka michache, ikiwa ni pamoja na kuanzisha huduma zake katika miji kadhaa barani Afrika, kampuni ya uber imekumbwa na mizozo kadhaa katika siku za karibuni, ikiwa ni pamoja na tuhuma za udhalilishaji wa kijinsia.
Wachambuzi wa masuala ya biashara za kimataifa wamesema kuna uwezekano mkubwa kwa Uber kupelekwa mahakamani na wadau, hususan wale walioathiriwa na uhalifu huo.
Kesi nyingi tayari zimewasilishwa mahakamani zikiishutumu kampuni hiyo kuhusiana na masuala mbali mbali huku baadhi ya mamlaka za miji katika nchi mbali mbali ulimwenguni zikipinga kile zinazokiita ukiukaji wa kanuni za usafiri.
Kampuni hiyo bado inashikilia rekodi ya kapuni za kibinafsi zilizo na dhamani kubwa Zaidi duniani. Ilikadiriwa kuwa na dhamani ya dola bilioni 68.

Mnangagwa:Ni enzi mpya ya demokrasia kamili Zimbabwe

Mtu anayetarajiwa kuwa rais mpya wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa alirejea nchini Zimbabwe jana Jumatano akitokea uhamishoni, na kulihutubia taifa akisema Zimbabwe imefungua ukurasa mpya wa demokrasia kamili.

Simbabwe Emmerson Mnangagwa in Harare (Reuters/M. Hutchings)
Emmerson Mnangagwa, Rais mtarajiwa wa Zimbabwe

Akiwahutubia mamia ya wafuasi wake katika makao makuu ya chama tawala nchini humo, ZANU-PF usiku wa Jumatano muda mfupi baada ya kurudi nchini, Emmerson Mnangagwa alisema ''leo tunashuhudia mwanzo mpya wa demokrasia kamili nchini mwetu.''
Ilikuwa kauli yake ya kwanza hadharani tangu tarehe sita Novemba, siku aliyofukuzwa na Robert Mugabe kutoka wadhifa wa Makamu wa Rais, katika mvutano wa kuwania nafasi ya kurithi madaraka ya urais, kati yake (Mnangagwa) na mke wa rais, Grace Mugabe.
Ni mvutano huo na mgogoro uliofuata, ambao ulilifanya jeshi kuingilia kati, na kuanzisha mchakato uliomlazimisha Rais Mugabe kusalimu amri na kuachia madaraka, baada ya kuzidiwa na shinikizo kutoka chama chake mwenye.
Arejea na heshima ya urais
Tangu wakati huo alikuwa akiishi uhamishoni nchini Afrika Kusini, na hapo jana alisafirishwa kwa ndege kurudi nyumbani, na kutua katika uwanja wa Manyame alikopokelewa na vigogo wa chama tawala, na kusafiri katika msafara wa magari mithili ya ule wa rais hadi Ikulu.
Katika hotuba yake kwenye makao makuu ya ZANU-PF ambayo ilirushwa moja kwa moja kwa njia ya televisheni, Mnangagwa alisisitiza umoja na haja ya kuufufua uchumi.
''Hakuna aliye muhimu kuliko mwingine, wote tuko wazimbabwe,'' amesema kiongozi huyo na kuongeza, ''tunataka kuukuza uchumi wetu, tunataka amani katika nchi yetu, na fursa za kazi, kazi, nchini mwetu...''
Simbabwe Mugabe und Mnangagwa ARCHIV 2009a (Getty Images/APF/A. Joe)
Ushirika wa muda mrefu kati ya Mnangagwa na Mugabe unazusha mashaka juu ya uhalisia wa mabadiliko yanayokea nchini Zimbabwe
Hotuba hiyo ya Emmerson Mnangagwa ambaye si mgeni katika siasa za Zimbabwe ilipokelewa kwa hisia tofauti. Kwa vijana wasio na ajira kama Remigio Mutero ambaye ni mhitimu wa chuo kikuu katika teknolojia ya komputa, hotuba hiyo ilikuna pale panapowasha.
''Ilikuwa hotuba nzuri kabisa, tunachotaka ni fursa za ajira'', alisema Mutaro baada ya kumsikiliza Mnangagwa.
Lakini Edgar Mapuranga, mwajiriwa katika sekta ya ulinzi wa mali binafsi, alisema haoni tofauti kati ya Mnangagwa na mtangulizi wake.
''Robert Mugabe ameondoka, lakini sioni Mnangagwa akifanya chochote tofauti na mkongwe huyo. Haya sio mabadiliko niliyoyatarajia, lakini ngoja tumpe muda'', alisema Mapuranga.
Watakaonufaika ni wale wale
Mjumbe maalumu wa Kansela Angela Merkel wa Ujerumani barani Afrika, Guenther Nooke, amesema ingawa Mnangagwa anatarajiwa kushinda katika uchaguzi ujao bila taabu, huo utakuwa ushindi wa kundi lile lile lililokuwa na ushawishi chini ya Mugabe, kwa kusaidiwa na China.
''Atapata ushindi kwa kutumia hila na vitisho, na kisha, tutashuhudia madaraka yakihama kutoka kiongozi mmoja wa kiimla, na kuangukia mikononi mwa mwingine wa aina hiyo'', amesema mjumbe huyo wa Kansela Merkel.
Robert Mugabe (picture-alliance/AP/T. Mukwazhi)
Azma ya Mugabe kumrithisha madaraka mkewe Grace ndiyo imemponza
Mnangagwa ambaye amekuwa mshirika wa karibu wa Robert Mugabe tangu enzi za kupigania uhuru, anaandamwa na tuhuma za kuhusika katika visa vingi vya ukiukaji wa haki za binadamu vilivyofanywa na serikali ya Robert Mugabe, vikiwemo uchakachuaji wa matokeo ya uchaguzi, na ukandamizaji wenye umwagaji mkubwa wa damu dhidi ya vuguvugu la upinzani wa watu wa kabila la Ndebele. Binafsi anatajwa kuwa mtu mwenye msimamo mkali na asiye na huruma.
Mshauri mkuu wa Shirika la Kimataifa la Kushughulikia Mizozo - ICG Kusini mwa bara la Afrika Piers Pigou, amesema doa hilo la siku za nyuma halitafutika katika mustakabali wa Mnangagwa. ''Litamfuata kokote aendako kama pande la Chingamu lililonasa katika unyayo wa kiatu chake'', amesema Pigou.

Wazimbabwe wasubiri kuapishwa rais mpya

Baadhi ya wananchi wa Zimbabwe wakiondosha picha ya Rais Robert Mugabe ukutani mara baada ya kujiuzulu.
Wananchi wa Zimbabwe wanasubiri kuapishwa kwa rais mpya kufuatia hatua ya Robert Mugabe kujiuzulu kutoka katika nafasi hiyo.
Mugabe ambaye amemaliza utawala wake uliodumu kwa miaka 37 atakumbukwa kwa utawala wa mabavu.
Marekani imepokea kitendo cha Mugabe kuondoka madarakani kwa kutoa wito kwa nchi hiyo kufanya uchaguzi uliyokuwa huru na haki.
Wakati huohuo mitaa ya Harare, mji mkuu wa Zimbabwe, ilikuwa imefurika watu waliokuwa wakisherekea kuondoka kwa kiongozi huyo.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari nchini Zimbabwe makundi ya watu walionekana wakishangilia katika mitaa ya Harare wakati habari zikienea kuwa Rais Robert Mugabe alikuwa amejiuzulu baada ya kutawala kwa miaka arubaini.

Spika wa Bunge la Zimbabwe Jacob Mudenda alisoma kile alichosema ni barua iliyokuwa imetoka kwa Rais Mugabe akitangaza rasmi kujiuzulu.

Wakati baadhi ya watu wanamchukulia Mugabe kuwa ni kiongozi ambaye alipigania uhuru wa Zimbabwe, watu wengine walikuwa na furaha kuona utawala wake unafikia kikomo.

“Sisi Wazimbabwe tunafuraha” na mtu mwengine alisema “ tunasherekea uhuru wetu.”Utawala wake, baadhi ya wachambuzi wanasema, uliiangamiza Zimbabwe.
“Ukiangalia nchi ambayo ilikuwa na uchumi imara, na kiwango bora kabisa cha elimu na mfumo wa afya, ni iliyokuwa na wasomi wa juu na wataalamu. Alichokifanya Mugabe kwa kujiuzulu kwa ajili ya uchumi, kwa dhana ya mapinduzi yaliyokubalika na wengi na kuzuilia demokrasia ni kitendo kiovu sana.
Wengine wamesema Mugabe angeweza kuepusha kufikia mwisho huu kama angeliamua kuachia madaraka mapema.

Lebanon: Hariri asitisha kujiuzulu kwake

Waziri Mkuu wa Lebanon Saad al Hariri amesitisha uamuzi wake wa kujiuzulu baada ya kurejea nchini kwake na kushiriki gwaride la Siku ya Uhuru,

Libanon Premier Hariri zeigt sich in Öffentlichkeit (Reuters/M. Azakir)
Muda mfupi  baada ya kurejea mjini Beirut, Hariri alikutana na Rais Michel Aoun, ambaye tangu mwanzo alikataa kukubali kujiuzulu kwa waziri huyo mkuu, akimtaka kwanza arejee nyumbani Lebanon. Na katika hotuba yake mbele ya umati mkubwa wa wafuasi wake waliokusanyika nje ya nyumba yake katika mji wa Beirut, Hariri aliahidi kuwa atabakia nchini Lebanon ili kulinda utulivu wa nchi hiyo.
Waziri mkuu wa Lebanon Hariri akiwaili kwenye sherehe za uhuru (Reuters/M. Azakir)
Waziri Mkuu wa Lebanon Saad Hariri
Hariri aliwaambia wafuasi wake kwamba alipowasilisha waraka wake wa kujiuzulu, rais alimwomba afanye subira ili kwanza kufanyike mashauriano zaidi kutokana na sababu zake na pia kwa kutazama historia ya kisiasa. Hariri alikubali ombi la rais Aoun.  Amesema ana matumaini kuwa yataanzishwa majadiliano ambayo yatazingatia Mkataba wa Taif na msingi wa makubaliano ya kitaifa, ambayo pia yatazingatia masuala ya kutofautiana baina yao na matokeo yake juu ya uhusiano wa Lebanon na ndugu zao wa nchi za Kiarabu.Lebanon ilipatwa na mshtuko kutokana na hatua ya ghafla ya kujiuzulu kongozi huyo mnamo tarehe 4 Novemba akiwa Saudi Arabia na baadaye nchi hiyo iliyumba kutokana na Hariri kuendelea kubakia nchini Saudi Arabia muda mrefu baadaye.
Mfalme wa Saudi Arabia Salman bin Abdulaziz Al Saud na waziri mkuu wa Lebanon Saad al-Hariri mjini Riadh (Reuters/Saudi Press Agency)
Waziri Mkuu wa Lebanon Saad Hariri na mfalme wa Saudi Arabia Salman bin Abdulaziz Al Saud
Kujiuzulu kwake kulionekana kama ni sababu ya kuuchochea mvutano kati ya mahasimu wakubwa na wababe wa wa muda mrefu wa eneo hilo, Saudi Arabia na Iran, hatua ambayo ilisababisha kuongezeka kwa hofu kwamba Lebanon ingekwama kutokana na mvutano huo wa kikanda. Wachambuzi wa mambo wanasema hatua ya leo ya Hariri kulifuta tamko lake la awali la kujiuzulu siku moja tu baada ya kurejea Lebanon ni kama kuitia aibu Saudi Arabia ambayo kwa kiasi kikubwa inaonekana kuwa ndiyo iliyochochea kiongozi huyo kujiuzulu.
Katika maneno yake yaliyoashiria mapatano baada ya kutoka kwenye makaazi ya Rais Aoun, Hariri alisema anayaweka maslahi ya Lebanon kwanza kabla ya kitu chochote kile, huku akitarajia mahusiano mazuri baina ya vyama vyote vya kisiasa kwa ajili ya kuyapa nguvu matumaini ya Lebanon. Siku ya Jumatano Waziri Mkuu huyo alishiriki katika sherehe za uhuru wa Lebanon ikiwa ni mara yake ya kwanza kushiriki katika hafla ya kitaifa tangu alipotangaza kujiuzulu.

Wednesday, November 22

MWANAFUNZI WA CHUO CHA UHAZILI TABORA AKUTWA AMEJINYONGA KWA KUTUMIA TAI


MWANACHUO mmoja Chuo cha Utumishi wa Umma –Tawi la Tabora kinachojulikana kama Uhazili  Raphael Kadesha (22)  amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia tai ya kuvaa shingoni.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Graifton Mushi tukio hilo limetokea jana saa 4 asubuhi ambapo marehemu alifunga tai juu ya kitanda chake.

Alisema kuwa marehemu alikuwa akisoma kozi cha Cheti cha Awali cha Utawala katika Chuo hicho.

Mushi aliongeza kuwa chanzo cha kifo hicho hakijulikani na Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kujua nini kilimfanya mwanachuo huyo kuchukua maamuzi hayo yaliyoacha simanzi katika jamii yake na Chuo kwa ujumla.

Alitoa wito kwa wanachuoni kuomba ushauri kwa viongozi wao Chuo au wa kiroho pindi wanapokuwa na matatizo binafisi kwani kujiua sio suluhisho la matatizo bali ni kuwaongezea walezi wao shida na majonzi zaidi.
Mushi alisema kuwa mwili wa marehemu umehifahiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kitete.

Naye Mkurugenzi wa  Chuo hicho Dkt. Ramadhani Marijani alitoa wito kwa wanachuo kuwa watulivu wakati Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi wa sababu zilizopelekea mwanachuo huyo kuchukua maamuzi yaliyoacha simamazi sio tu kwa familia yake bali hata kwa Jumuiya nzima ya Uhazili.

Alisema kuwa ni vema kama kuna mwanachuo yoyote anakuwa na tatizo au msongo wa mawazo kuwaeleza viongozi wake wawe wa Serikali ya Wanafunzi, Mama Mlenzi, Mshauri wa Wanachuo au Mkurugenzi mwenye ili waweze kusaidia katika ushauri utakaowapa ufumbuzi kuliko kuchukua maamuzi ya haraka.