Ufaransa imetoa wito wa kufanyika mkutano katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kujadili vitendo vibaya wanavyofanyiwa Wahamiaji nchini Libya.
Hatua hiyo imekuja baada ya taarifa kutoka nchini Libya kusema kuwa Wahamiaji wa Kiafrika wamekuwa wakiuzwa kama watumwa.
Baada ya mkutano wake na Kiongozi wa Umoja wa Afrika, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amekuelezea kuuzwa huko kama uhalifu dhidi ya ubinadamu na kuongeza kuwa hatua zaidi zinahitajika kuchukuliwa kuvunja mtandao wa watu wanaohusika na biashara haramu ya binadamu.
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian amesema vikwazo vya kimataifa vinapaswa kuwekwa iwapo mamlaka za Libya hazitachukua hatua, kupiga marufuku vitendo hivyo.
No comments:
Post a Comment