Kimya kirefu cha rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma pamoja na chama chake tawala cha ANC kufuatia kujiuzulu kwa Robert Mugabe kinashangaza.
Kinaonyesha ushawishi wa kisaikolojia aliyokuwa nao kwao na walishangazwa sana na hatua aliyochukua.
Kile afisi ya rais Zuma ilichosema ni kwamba hatoweza tena kuelekea nchini Zimbabwe kama alivyokuwa amepanga ili kupatanisha kbal ya rais Mugabe kutangaza kujiuzulu.
Ziara hiyo sasa imeahirishwa hadi tyangazo jingine , taarifa ilisema.
Lakini badala yake chma cha upinzani nchini Afrika Kusini DA kilijibu na hivyobasi kuungwa mkono na raia weusi pamoja na wazungu kiliposema:
Huu ni ushindi wa raia wa Zimbabwe ambao wametaabika chini ya uongozi wa Mugabe .Habari ya bwana Mugabe sio geni na kwamba inaendelea katika bara la Afrika.Mtu aliyekuwa shujaa wa taifa lake , Mugabe alisababisha migawanyiko, ukosefu wa udhabiti na kuharibika kwa uchumi wakati alipobadilika kutoka kuwa mpiganiaji wa uhuru hadi kuwa dikteta.Hilo sio tu kwa Mugabe bali hata Zanu -PF chama ambacho amekitawala kwa kutumia nguvu kwa kuchukua mamlaka tangu taifa hilo lijipatie Uhuru.Chama cha ANC kinaonyesha ishara kama zile za Zanu-PF, kimekumbwa na ufisadi mkubwa na ghasia huku pande pinzani zikipigania madaraka katika serikali kwa lengo la kujitajirisha badala ya kuwahudumia wananchi.Baada ya kuchukua madaraka miaka 23 kutoka kwa wazungu ,ANC sasa kinakabiliwa na changamoto ya kujiimarisha au tishio la kuangamiza uchumi wa Afrika kusini kama Zanu-Pf kilivyofanya kwa miaka 37.
No comments:
Post a Comment