Haki miliki ya pichaEPAImage captionPolisi watibua jaribio la pili la shambulizi mjini Cambrils Uhispania
Maafisa wa polisi wa Uhispania wanasema kuwa wamewaua watu watano katika mji wa Cambrils ili kuzuia jaribio la pili la shambulio baada ya shambulio la hapo awali kufanyika mjini Barcelona.
Washambuliaji walikuwa wamevalia vilipuzi , polisi wamesema.
Watu 13 walifariki huku makumi wakijeruhiwa baada ya gari dogo kuingia katika eneo la watu mjini Barcelona eneo la Las Ramblas siku ya alhamisi mchana
Mamlaka sasa wanahusishwa shambulio hilo la Barcelona pamoja na lile la Camrils huku mlipuko ukiripotiwa katika nyumba moja siku ya Jumatano jioni katika mji wa Alcanar ambapo mtu mmoja alifariki.
Awali afisa mkuu wa polisi Josep Lluis Trapero alisema kuwa inaonekana wakaazi wa eneo la nyumba ya Alcanar walikuwa wakiandaa kuntengeza kilipuzi .
Mjini Cambrils watu saba akiwemo afisa mmoja wa polisi alijeruhiwa wakati gari lilipovurumishwa katika umati wa watu mapema siku ya Ijumaa kulingana na huduma za dharura huko Catalan.
Mtu mmoja yuko katika hali mahututi.
Vyombo vya habari vya Uhispania viliripoti kwamba washambuliaji waliuawa wakati walipojaribuo kutoroka baada ya gari lao kupinduka.Baadaye misururu ya milipuko ilifuatia.
Haki miliki ya pichaAFPImage captionMaandamano ya kupinga dhuluma za kingono dhidi ya watoto India
Msichana wa umri wa miaka 10 ambaye alinyimwa ruhusa ya kuavya mimba na mahakama ya juu zaidi nchini India mwezi uliopita amejifungua mtoto msichana.
Msichana huyo hajafahamu kuwa amejifungua. Wakati akiwa na uja uzito aliambiwa kuwa tumbo lake kubwa lilitokana na jiwe kubwa lililokuwa ndani ya tumbo.
Mtoto huyo mwenye uzito wa kilo 2.5 alizaliwa kwa njia ya upasuaji katika hospitali ya Chandigarh.
Mama na mtoto wote wako hali nzuri, afisa mmoja aliiambia BBC.
Msichana huyo anadaiwa kubakwa mara kadha katika kipindi cha miezi saba iliyopita na mjomba wake ambaye wa sasa amekamatwa.
Mimba yake iligunduliwa karibu mwezi mmoja uliopita wakati alilalamikia maumivu ya tumbo na wazazi wake wakampeleka hospitalini.
Mwezi uliopita mahakama ya juu ilikataa kumruhusu kuavya mimba hiyo kwa misingi kuwa alikuwa mdogo sana kuwa mjamzito, baada ya madaktari kusema kuwa kuavya mimba hiyo ya wiki 32 yaweza kuhatarisha maisha yake.
Haki miliki ya pichaAFPImage captionDangote anaorodheshwa kuwa mtu tajiri zaidi Afrika
Mfanyabiashara tajiri raia wa Nigeria Aliko Dangote, ambaye anaorodheshwa kuwa mtu tajiri zaidi Afrika, amesema kuwa atamfuta kazi meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, ikiwa atafaulu kuinunua klabu hiyo ya Uingereza, kwa mujibu wa shirika la Bloomberg.
Wakati wa mahojiano na shirika hilo, Bwana Dangote alisema kuwa atajaribu kununua klabu hiyo, wakati ujenzi wa kiwanda chake cha kusafisha mafuta cha gharama ya dola bilioni 11 mjini Lagos utakamilika.
Bw. Dangote anasema amekuwa shabiki wa Arsenal tangu miaka 1980.
Wenger ni mmoja wa mameneja wa kandanda wanaosifika sana barani Ulaya na hivi majuzi, alisaini mkataba wa miaka miwili na kuendelea kuwa na klabu hiyo kwa zaidi ya miongo miwili.
Kuna maoni tofauti kutoka kwa wafuasi wake, wengine wakisema kuwa klabu hiyo inahitaji meneja mpya ili kiweze kurejea hadhi yake.
Serikali ya Catalonia imesema watu 13 wamekufa na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa baada ya gari la mizigo kugonga watu katika eneo la watalii la Las Ramblas, Barcelona.
Polisi nchini Uhispania wanasema kuwa watu kadhaa wamejeruhiw watoa huduma za dharura wakiwashauri watu kukaa mbali na eneo hilo.
Ripoti kutoka eneo hilo zinasema kuwa watu wanajificha ndani ya maduka yaliyo karibu.
Shirika la hahari la Reuters linasema kuwa watoa huduma za dharura wameomba kusitishwa kwa huduma za usafiri wa mabasi na kufungwa vituo vya treni.
Gazeti la El Pais lilisema kuwa dereva wa gari aliliendesha na kutoroka kwa miguu baada ya kuwagonga watu kadha.
Image captionShirika la hahari la Reuters linasema kuwa watoa huduma za dharura wameomba kusitishwa kwa huduma za usafiri wa mabasi na vituo vya treni.
"Watu kwenye ofisi yangu waliona gari likiendeshwa kwenda kwa umati wa watu huko Las Ramblas," alisema mtu moja anayefanya kazi sehemu hiyo.
"Niliona karibu watu wawili au watatu hivi wakilala chini.
"Kuna magari kadha ya kubeba wagonjwa na polisi waliojihami wakiwa na bunduki kwa sasa," alisema.
Taarifa za kina kuhusu kisa hiki bado hazipo lakini magari yashatumiwa kugonga watu kwenye misururu ya mashambulizi barani Ulaya tangu mwezi Julai mwaka uliopita.
Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionMaeneo ya milimani ndio yaliyoathirika zaidi
Wiizara ya afya nchini Sierra Leone imesema takriban nusu ya maiti 400 zitokanazo na maporomoko ya udongo na mafuriko nje ya mji wa Freetown tayari zimezikwa.
Serikali ilisema mazishi ya pamoja yangeahirishwa hadi leo ili kutoa fursa kwa ndugu na jamaa kutambua miili ya maiti ya waathirika.
Lakini mkuu wa wataalamu wa magonjwa kutoka mjini Freetown ameiambia BBC kwamba baadhi ya mazishi yalikuwa yamefanyika.
Imefahamika kuwa mazishi hayo yamehusisha miili ambayo tayari ilitambuliwa au ilikuwa imeharibika kabisa.
Watu wapatao mia sita mpaka sasa bado hawajulikani walipo.
Rais wa Sierra Leone ametangaza siku saba za maombolezi.
Nathaniel Williams ni daktari katika hospitali kuu ya Connaught, iliyopo Freetown, anasema hivi sasa kuna tahadhari kubwa ya kutokea magonjwa ya milipuko kama vile kipindupindu.
Ameongeza kusema kuwa hivi sasa kunahitajika madawa na vyakula, kwa wale walioathirika.
Hata hivyo, Umoja wa Mataifa nchini humo umesema tayari umeweka mikakati ya kuweza kukabiliana na magonjwa ya milipuko iwapo yatatokea.
Haki miliki ya pichaEPAImage captionAhmad al-Faqi al-Mahdi alihukumiwa kifungo cha miaka 9 na ICC
Mwanamgambo mmoja wa kiislamu ambaye anatumikia kifungo gerezani kwa kuharibu maeneo ya kitamaduni mjini Timbuktu nchini Mali, ameamrishwa kulipa dola milioni 3 kwa uharibifu huo.
Ahmad al-Faqi al-Mahdi alihukumiwa kifungo cha miaka 9 na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC.
Alikiri kuongoza waasi ambao waliharibu maeneo ya kitamaduni nchini Mali mwaka 2012.
Uamuzi huo wa hivi punde wa majaji kwenye mahakama ya ICC unakuja baada ya kutathmini vile waathirwa wake watafidiwa.
Jaji Raul Cano Pangalangan alisema kuwa dola milioni 3 zitaenda kwa jamii ya Timbuktu inayolinda maeneo hayo.
Haki miliki ya pichaAFP/ GETTY IMAGESImage captionMaeneo tisa ya kitamaduni yalihabiwa mwaka 2012
Huku Mahdi akiwa gerezani na bila pesa , fedha hizo zitatoka kwa mfuko wa ICC unaoshughulokia waathiriwa.
Mahdi ambaye alitajwa kuwa msomi wa dini kwenye stakabadhi za mahakama, aliongoza waasi kuharibu maeneo 9 ta kitamaduni.
Waendesha mashtaka walisema kuwa Bw. Mahdi alikuwa mwanachama wa kundi la kislamu wa kundi la Ansar Dine lililo na uhusiano kundi la al-Qaeda.
Zaidi ya watu 40 wameuawa kwenye janga la maporomoko ya ardhi kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.
Wengi wa wale waliouawa ni kutoka kijiji kimoja kinachofanya uvuvi katika kingo za ziwa Albert.
Mvua kubwa imesababisha sehemu za mlima ulio karibu kuporomoka na kufunika kijiji hicho kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.
Watu wengine kadhaa walifariki wakitafuta dhahabu kwenye migodi ya zamani.
Kumekuwa na majanga mabaya ya maporomo ya ardhi mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo miaka ya hivi karibuni.
Janga hili linatokea baada ya mafuriko mabaya yaliyotekea kwenye mji wa Freetown nchini Sierra Leone siku ya Jumatatu ambapo zaidi ya watu 300 waliuawa.
Ripoti zinasema kuwa watu 28 walizikwa jana huku 12 wengine wamezikwa leo.
Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionRais Mugabe na mkewe bi Grace Mugabe
Maafisa wa polisi wa Afrika Kusini wametoa tahadhari dhidi ya Mkewe rais Mugabe katika mipaka ya taifa hilo , waziri wa polisi nchini humo amesema.
Ametuhumiwa kwa kumpiga na kumjeruhi mwanamke wa miaka 20 katika kichwa chake katika chumba cha hoteli karibu na mji wa Johannesburg .
Polisi wanatariaji kwamba Bi Mugabe mwenye umri wa miaka 52 alipaswa kujiwasilisha mbele yao siku ya JUmanne lakini akakataa kufanya hivyo.
Bi Grace mugabe kwa sasa hajulikani yu wapi lakini inaaminikwamba bado yupo Afrika Kusini.
Image captionGabnriela Engels
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe pia amewasili nchini Afrika Kusini kwa kikao cha viongozi wa mataifa ya Afrika Kusini SADC unaotarajiwa kuanza siku ya Ijumaa.
Bi Mugabe hajatoa tamko lolote kuhusu madai hayo.
Waziri wa polisi Fikile Mbalula alisema: Sisi polisi wa Afrika Kusini tayari tumeweka notisi katika mipaka yetu yote ili kumzuia bi Mugabe kuondoka nchini siku ya Jumatano, wakili wa Afrika Kusini Gerrie Nel aliyefanikiwa kumshtaki mwanariadha mlemavu Oscar PIstorius anamuunga mkono mwanamke anayemtuhumu bi Mugabe kwa kumpiga, Gabriela Engels.
Bwana Nel sasa anashirikiana na kundi la Afriforum ambalo linapigania haki za Afrikaners nchini Afrika Kusini.
Kundi hilo limesema kuwa iwapo polisi watashindwa kuchukua hatua katika kesi hiyo basi litamshtaki bi Mugabe.
Haki miliki ya picha
Pia limesema kuwa litakabiliana na hatua yoyote ya kumpatia kinga ya kidiplomasia bi Mugabe.
Bi Engels aliambia BBC kwamba alishambuliwa na bi Mugabe aliyeamini kwamba alikuwa akijua kule aliko mwanawe Bellarmine.
''Tuliendelea kumwambia hatujui aliko...hatujamuona usiku wote...alinikamata na kuanza kunipiga.Nakumbuka nikianguka katika sakafu na damu nyingi katika uso na shingo yangu.Alitupiga akiwa na chuki nyingi'', alisema msichana huyo..
Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionBi Engels Gabriella aliyeshambuliwa na bi Grace Mugabe
Familia ya mwanamke aliyedaiwa kushambuliwa na bi Grace Mugabe imedaiwa kufuatwa na kuombwa na mtu asiyejulkani kukubali fedha kama fidia ya kutupilia mbali kesi hiyo , wakili wake amesema.
Familia haitaki kufanya hivyo, Gerrie Nel alisema.Walisema tuzungumze na tuwache kesi hii, lakini hakuna kiwango cha fedha kilichotajwa ,aliongezea.
Bwana Nel anajulikana kwa jina la utani kama ''the Pitbull''. Alifanikiwa kumshtaki mwanariadha mlemavu Oscar Pistorius kwa mauaji.
Wakati huohuo katika mahojiano marefu ya simu na bi Gabriella Engels ambaye amemtuhumu bi Grace Mugabe kwa kumpiga, Mwandishi wa BBC Pumza Fihlani alitulia na kuonekana kuwa mtu aliyekuwa na wasiwasi mwingi mara kwa mara.
Akielezea tukio hilo bi Engels mwenye umri wa miaka 20 alisema kuwa yeye na watu wengine wanne, wawili wakiwa wana wa kiume wa rais Mugabe na bi Grace Mugabe walikuwa wakinywa vinywaji siku ya Jumapili usiku katika chumba kimoja cha hoteli mjini Sandton, makaazi ya kifahari yaliopo Johannesburg.
Baadaye alienda katika chumba chengine na bi Mugabe akamfuata akiwatafuta wanawe.
Bi Mugabe alikuwa ameshikilia waya wa umeme mkononi mwake....alinizuia na kuanza kunipiga .
Nilijiangusha chini na kuanza kubingirika ili kukwepa kichapo hicho, na ni hapo aliponipiga na waya hiyo. Na nakumbuka nikiwa katika sakafu huku nikiwa nimejaa damu usoni na shingoni, bi Engels alidai.
Nilikuwa nikifikiria nitoke katika chumba hicho kabla ya mwanamke huyu kuniuwa.
Watu waliokuwa katika chumba hicho ni walinzi wake na walikuwa wamesimama nyuma yake huku akitupiga.
Tulimsihi kuwacha kufanya hivyo ,lakini hakutaka kusikia aliendelea kutupiga...alitupiga akiwa na chuki nyingi .
Sielewi kwa nini alitushambulia hivyo.
Haki miliki ya pichaAFPImage captionBi Grace Mugabe
Hadi leo marafiki zangu sielewi kwa nini mwanamke huyu alitushambulia vile bila ya sababu yoyote, Engels aliongezea.
kabla nitambue alikuwa bi Mugabe, nilijua nilifaa kumshtaki kwa kunishambulia kwa kuwa nilijeruhiwa vibaya
Sikujua yeye ni nani. na nilipojua yeye ni nani, sikutaka kumshtaki .. lakini mamangu akanisukuma kuwasilisha mashtaka hayo mahakamani, kwa sababu aliniambia: Kile mwanamke huyu alichotenda sio sawa.
Hatuwezi kuruhusu kukwepa kitendo alichofanya, alisema bi Engels.
Mwanamke huyo wa miaka 20 alisema: Ningefurahia sana iwapo angepelekwa jela.. hilo ndio lengo langu kwa sasa.
Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi, Agosti 17, Meneja kituo kikuu cha utabiri, Samwel Mbuya amesema manyunyu na mvua zinazoonekana zimesababishwa na mabadiliko ya mfumo wa hali ya hewa kama ambavyo taarifa ya hali ya hewa ya mamlaka hiyo ya Juni ilieleza.
Dar es Salaam. Kufuatia kuendelea kwa mvua za hapa na pale jijini Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imesema mvua hizo haziwezi kusababisha madhara kwani zinatokana na mabadiliko tu ya muda mfupi.
Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi, Agosti 17, Meneja kituo kikuu cha utabiri, Samwel Mbuya amesema manyunyu na mvua zinazoonekana zimesababishwa na mabadiliko ya mfumo wa hali ya hewa kama ambavyo taarifa ya hali ya hewa ya mamlaka hiyo ya Juni ilieleza.
Amesema Mamlaka ya Hali ya Hewa itaendelea kutoa taarifa za hali na mwenendo wa mvua hizo ili kusaidia jamii kupata taarifa muhimu kuhusiana na maendeleo ya hali ya hewa.
Ameongeza kuwa sambamba taarifa hizo mamlaka itatoa taarifa ya utabiri wa mvua za vuli 2017 mwishoni mwa Agosti 2017.
Akizungumza leo Alhamisi, Agosti 17 jijini Dar es Salaam, Mkemia Mkuu wa Serikali, Samwel Manyele amesema ongezeko hilo linatokana na waagizaji wengi kuagiza mzigo wa kemikali bila kufuata sheria.
Dar es Salaam. Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali imesema imelemewa na kiwango kikubwa cha kemikali za matumizi ya nyumbani na viwandani zinazoingizwa nchini kwa siku.
Akizungumza leo Alhamisi, Agosti 17 jijini Dar es Salaam, Mkemia Mkuu wa Serikali, Samwel Manyele amesema ongezeko hilo linatokana na waagizaji wengi kuagiza mzigo wa kemikali bila kufuata sheria.
Amesema kabla ya mwaka 2013 walikuwa wakitoa vibali vitano hadi saba kwa siku, lakini kuanzia mwaka huo wamekua wanatoa vibali 100 hadi 150 kwa siku huku wakilazimika kufanya kazi saa 24.
"Sheria inamtaka muagizaji wa kemikali kuomba kibali, kusajiliwa kabla ya kuagiza mzigo, lakini walio wengi wanakiuka sheria kwa kuagiza mzigo ukiwa bandarini ndiyo wanaanza kuomba nyaraka hizo muhimu," amesema Profesa Manyele.
Profesa Manyele amesema mrundikano wa mizigo unakuwa mkubwa kutokana na kuwa na wafanyakazi wasiofika 100 nchi nzima.
"Kuna vituo vingi vya kupokelea kemikali, ndani ya bandari vipo sita na nje vipo 17.
" Kutokana na wingi huo wakaguzi wanalazimika kutumia muda mwingi kutembea kufuata mizigo ilipo,"amesema Profesa Manyele.
Mbeya. Polisi wameimarisha ulinzi kuzunguka soko la Sido ambalo limeteketea kwa moto kwa lengo la kuwazuia wafanyabiashara kuendelea n ujenzi wa vibanda vya kudumu.
Polisi wamezunguka eneo la soko tangu usiku wa kuamkia Leo wakiwa na silaha za moto na mabomu ya machozi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mohammed Mpinga ametoa sababu mbili za kumwaga polisi wengi eneo hilo akidai kwamba wanatekeleza agizo la Serikali kuwazuia wafanyabiashara hao kujenga vibanda hivyo hadi watakapopata kibali .
Pia amesema wanazuia msongamano wa watu ndani ya soko hilo ili kutoa nafasi nzuri kwa kamati iliyoundwa na kamati ya ulinzi na usalama ya kuchunguza chanzo cha moto huo na hasara iliyojitokeza ili kufanya kazi hiyo kwa uhuru zaidi.
Mkapa ambaye ujumbe wake uko nchini Burundi kwa ajili ya mazungumzo na Serikali ya nchi hiyo katika jitihada za kusuluhisha mzozo wa kisiasa aliwasili jana mjini Kigali akiwa miongoni mwa viongozi zaidi 20 ambao wanahudhuria sherehe hizo.
Dar es Salaam.Rais mstaafu wa Tanzania, Benjamin Mkapa ni miongoni mwa viongozi mbalimbali wa Afrika wanaohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Rwanda, Paul Kagame aliyeshinda katika uchaguzi uliofanyika Agosti 4.
Mkapa ambaye ujumbe wake uko nchini Burundi kwa ajili ya mazungumzo na Serikali ya nchi hiyo katika jitihada za kusuluhisha mzozo wa kisiasa aliwasili jana mjini Kigali akiwa miongoni mwa viongozi zaidi 20 ambao wanahudhuria sherehe hizo.
Sherehe hizo ambazo zinatarajiwa kupambwa na burudani mbalimbali zinafanyika katika Uwanja wa Taifa wa Amahoro. Rais Kagame atakuwa anaanza muhula wa kwanza wa miaka saba tangu taifa hilo lilipofanyia marekebisho katiba yake.
Miongoni mwa viongozi wa Afrika wanaohudhuria sherehe hizo ni pamoja na Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Faustin-Archange Touadera ambaye alikuwa wa kwanza kuwasili nchini humo.
Wengine ni Rais wa Kenya, Uhuru Kenya, Rais wa Djibouti, Ismail Omar Guelleh, Rais wa Niger, Mahamadou Issoufou, Rais wa Senegal, Macky Sally, Rais wa Zambia, Edgar Lungu na Rais wa Congo Brazaville, Sassou Nguesso
Ni baada ya askari kuweka doria huku wakiwa wameshika silaha za moto na mabomu ya machozi
Mbeya. Wafanyabiashara wa Sido wameanza kujikusanya kwenye vikundi baada ya kuzuiliwa kuendelea na ujenzi wa vibanda vya kudumu ndani ya soko hilo ambalo limeteketea kwa moto.
Shughuli nyingine maeneo ya Mwanjelwa, Kabwe zimesimama maduka yamefungwa kuhofia usalama wa Mali zao.
Mwenykiti wa wafanyabiashara wa soko la Sido, Charles Syonga amesema kwa sasa wanasubiriana wajumbe wa bodi ya Soko hilo kuona nama ya kufanya na kuwambia wafanyabiashara wafanye nini kutokana na hali ilivyo sasa.
‘'Tunashindwa kuelewa kinachoendelea, sisi hapa Jana jioni tuliweka ulinzi ktk soko hili lakini usiku polisi wakafika wakiwa doria na wakawatoa watu waliokuwa ndani ya soko, na Leo asubuhi sote tumekuja hapa na kukuta polisi wametanda soko lote, na hatujapata taarifa yoyote toka serikalini wala hakuna kiongozi wa kiserikali aliyefika kuzungumza na wafanyabiashara'. alisema Syonga
Viongozi wa dini wa kikristo na kiislam wa mkoani Arusha waliwaombea watoto.
Kilimanjaro. Furaha imetawala ujio wa watoto watatu wa Shule ya Lucky Vicent waliowasili leo Ijumaa, Agosti 18 wakitokea nchini Marekani kwenye matibabu baada ya kupata ajali Mei mwaka huu.
Wazazi na ndugu waliruhusiwa kuingia ndani ya ndege hiyo kuwapokea watoto wao ambao wamepata nafuu kwa kiasi kikubwa.
Wilson Tarimo alikuwa wa kwanza kushuka katika ndege akiambatana na mdogo wake aliyeingia katika ndege kwa ajili ya kumpokea.
Baada ya hapo aliyefuatia ni Saidia Awadhi pili akifuatana na Doreen Mshana kushuka katika ndege hiyo iliyokuwa na wajumbe 16 ambao waliambatana na watoto hao.
Baada ya kushuka walipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira aliyeambata na viongozi wengine kutoka Mkoa wa Arusha.
Watoto hao wote wakati wanashuka walionekana wenye nyuso za furaha baada ya kukaa Marekani kwa miezi mitatu wakipata matibabu.