Friday, August 18

Polisi watibua jaribio la pili la shambulizi Uhispania

Polisi watibua jaribio la pili la shambulizi mjini Cambrils UhispaniaHaki miliki ya pichaEPA
Image captionPolisi watibua jaribio la pili la shambulizi mjini Cambrils Uhispania
Maafisa wa polisi wa Uhispania wanasema kuwa wamewaua watu watano katika mji wa Cambrils ili kuzuia jaribio la pili la shambulio baada ya shambulio la hapo awali kufanyika mjini Barcelona.
Washambuliaji walikuwa wamevalia vilipuzi , polisi wamesema.
Watu 13 walifariki huku makumi wakijeruhiwa baada ya gari dogo kuingia katika eneo la watu mjini Barcelona eneo la Las Ramblas siku ya alhamisi mchana
Mamlaka sasa wanahusishwa shambulio hilo la Barcelona pamoja na lile la Camrils huku mlipuko ukiripotiwa katika nyumba moja siku ya Jumatano jioni katika mji wa Alcanar ambapo mtu mmoja alifariki.
Awali afisa mkuu wa polisi Josep Lluis Trapero alisema kuwa inaonekana wakaazi wa eneo la nyumba ya Alcanar walikuwa wakiandaa kuntengeza kilipuzi .
Mjini Cambrils watu saba akiwemo afisa mmoja wa polisi alijeruhiwa wakati gari lilipovurumishwa katika umati wa watu mapema siku ya Ijumaa kulingana na huduma za dharura huko Catalan.
Mtu mmoja yuko katika hali mahututi.
Vyombo vya habari vya Uhispania viliripoti kwamba washambuliaji waliuawa wakati walipojaribuo kutoroka baada ya gari lao kupinduka.Baadaye misururu ya milipuko ilifuatia.

No comments:

Post a Comment