Friday, August 18

Biashara zasimama Mbeya, hofu yatanda


Mbeya. Wafanyabiashara wa Sido wameanza kujikusanya kwenye vikundi baada ya kuzuiliwa kuendelea na ujenzi wa vibanda vya kudumu  ndani ya soko hilo ambalo limeteketea  kwa moto.
Shughuli nyingine maeneo ya Mwanjelwa, Kabwe zimesimama maduka yamefungwa kuhofia usalama wa Mali zao.
Mwenykiti wa wafanyabiashara wa  soko la Sido, Charles Syonga amesema kwa sasa wanasubiriana wajumbe wa bodi ya Soko hilo kuona nama ya kufanya na kuwambia wafanyabiashara wafanye nini kutokana na hali ilivyo sasa.
‘'Tunashindwa kuelewa kinachoendelea, sisi hapa Jana jioni tuliweka ulinzi ktk soko hili lakini usiku polisi wakafika wakiwa doria na wakawatoa watu waliokuwa ndani ya soko, na Leo asubuhi sote tumekuja hapa na kukuta polisi wametanda soko lote, na hatujapata taarifa yoyote toka serikalini wala hakuna kiongozi wa kiserikali aliyefika kuzungumza na wafanyabiashara'. alisema Syonga

No comments:

Post a Comment