
Mwanamgambo mmoja wa kiislamu ambaye anatumikia kifungo gerezani kwa kuharibu maeneo ya kitamaduni mjini Timbuktu nchini Mali, ameamrishwa kulipa dola milioni 3 kwa uharibifu huo.
Ahmad al-Faqi al-Mahdi alihukumiwa kifungo cha miaka 9 na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC.
Alikiri kuongoza waasi ambao waliharibu maeneo ya kitamaduni nchini Mali mwaka 2012.
Uamuzi huo wa hivi punde wa majaji kwenye mahakama ya ICC unakuja baada ya kutathmini vile waathirwa wake watafidiwa.
Jaji Raul Cano Pangalangan alisema kuwa dola milioni 3 zitaenda kwa jamii ya Timbuktu inayolinda maeneo hayo.

Huku Mahdi akiwa gerezani na bila pesa , fedha hizo zitatoka kwa mfuko wa ICC unaoshughulokia waathiriwa.
Mahdi ambaye alitajwa kuwa msomi wa dini kwenye stakabadhi za mahakama, aliongoza waasi kuharibu maeneo 9 ta kitamaduni.
Waendesha mashtaka walisema kuwa Bw. Mahdi alikuwa mwanachama wa kundi la kislamu wa kundi la Ansar Dine lililo na uhusiano kundi la al-Qaeda.
No comments:
Post a Comment