Sunday, April 1

Wabunge wanne waliopata ajali watoka hospitali


Dar es Salaam. Wabunge wanne kati ya sita waliokuwa wakipatiwa matibabu katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) wameruhusiwa kurejea nyumbani.
Ijumaa Machi 30,2018 wabunge hao walilazwa MOI baada ya kupata ajali walipokuwa wakitokea Dodoma kuelekea Dar es Salaam.
Ajali hiyo ilitokea eneo la Bwawani mkoani Morogoro, Alhamisi Machi 29,2018 saa mbili usiku na kabla ya kuhamishiwa MOI walipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Morogoro.
Meneja Ustawi wa Jamii na Uhusiano wa MOI, Almas Jumaa akizungumza na MCL Digital leo Aprili Mosi, 2018 amesema mbunge wa Makunduchi, Haji Ameir Haji anaendelea na matibabu akiwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).
Amesema Juma Othman Hija wa Tumbatu yupo wodini akiendelea na matibabu.

No comments:

Post a Comment