Sherehe za kuwashwa Mwenge zinatarajiwa kuanza saa moja asubuhi hadi saa tano asubuhi katika kiwanja cha Magogo mjini Geita.
Akizungumza na MCL Digital leo Jumapili Aprili Mosi,2018 Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel amesema viongozi kadhaa wamewasili akiwemo Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Jenista Mhagama.
Mwenge wa Uhuru ambao utakimbizwa mkoani Geita kwa siku sita utakabidhiwa mkoani Kagera Aprili 7,2018.
No comments:
Post a Comment