Sunday, April 1

Rais JPM awataka Watanzania kuishi kwa amani


Dar es Salaam. Rais John Magufuli amewataka Watanzania wote kuendelea kuishi kwa amani na upendo huku wakishiriki ipasavyo katika ujenzi wa Taifa.
Rais amesema hayo leo Aprili Mosi baada ya kuungana na Wakristo wote nchini katika maadhimisho ya Misa Takatifu ya Sikukuu ya Pasaka iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu  Joseph, Jimbo  Kuu la Dar es Salaam.
Rais Magufuli amesema: “Kifo na ufufuo wa Bwana Yesu Kristo ukafufue matendo yetu, tuendelee kuijenga amani yetu  upendo wetu na tujenge maendeleo ya Watanzania wote, wani Kristo amefundisha upendo miongoni mwetu.’’
 ‘’Kwa hiyo nakushukuru sana kwa kuongoza Misa hii naomba ufikishe shukrani zangu kwa kardinali Pengo, maaskofu wote na Watanzania wote tuendelee kusimama pamoja  ili kulijenga Taifa letu.’’ amesema Magufuli.

No comments:

Post a Comment