Askofu Nzigilwa amesema hayo leo Jumapili Aprili Mosi, 2018 wakati wa Misa Takatifu ya Pasaka katika Kanisa la Mtakatifu Petro, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Amewataka waumini kulipa ubaya kwa wema.
“Haijalishi umeumizwa na nini kutoka kwa watu wanaokuzunguka, usilipe ubaya huo kwa ubaya bali lipa ubaya kwa wema nawe utakuwa na amani," amesema.
Askofu Nzigilwa amesema ulimwengu umejaa mambo mengi yanayoumiza.
“Unaweza kutendewa ubaya mwingi kama vile kupigwa, kuonewa, kudhalilishwa na hata kuuawa. Ukifanyiwa ubaya kwa sababu ya wema wako kuwa na amani na mshukuru Mungu, lakini kama unafanyiwa ubaya kwa sababu ya dhambi uliyotenda basi tubu na Mungu atakusamehe na utakuwa na maisha ya amani," amesema.
Amesema Mkristu aliyeiva ni yule mwenye uwezo wa kushinda ubaya kwa kufanya yaliyo mema na ndiyo maisha wanayopaswa kuishi kama Wakristu.

No comments:
Post a Comment