Sunday, April 1

Rais mpya aapishwa nchini Botswana

Mokgweetsi Masisi(kushoto)Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMokgweetsi Masisi(kushoto)
Makamu wa rais wa Botswana, Mokgweetsi Masisi, ameapishwa kama rais katika sherehe iliyofanywa mji mkuu, Gaborone.
Masisi, ameshika hatamu kutoka kwa Rais Ian Khama, ambaye aliondoka madarakani jana, baada ya kuongoza kwa miaka 10.
Botswana itafanya uchaguzi mwaka ujao.Botswana ni ya pili kati ya nchi zinazochimba almasi nyingi kabisa.
Baada ya kuapishwa, Rais Masisi, alisema kuwa kupunguza ukosefu wa ajira kati ya vijana, ndio jambo muhimu kabisa kwake, na pia aliahidi kuyapa kipa-umbele, mapambano dhidi ya Ukimwi, utumizi mbaya wa ulevi na madawa ya kulevya, pamoja na rushwa.
Masisi, ameshika hatamu kutoka kwa Rais Ian Khama(kushoto)Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMasisi, ameshika hatamu kutoka kwa Rais Ian Khama(kushoto)

No comments:

Post a Comment