Sunday, April 1

Vita vya Syria: 'muafaka umekubaliwa' kuwaondoa watu waliojeruhiwa kutoka Douma

Muafaka umekubaliwa wa kuwaondoa watu waliojeruhiwa vibaya, kutoka katika ngome ya mwisho iliyokuwa ikishikiliwa na waasi katika mji wa Douma, huko Ghouta MasharikiHaki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
Image captionMuafaka umekubaliwa wa kuwaondoa watu waliojeruhiwa vibaya, kutoka katika ngome ya mwisho iliyokuwa ikishikiliwa na waasi katika mji wa Douma, huko Ghouta Mashariki
Duru kutoka Syria, zinasema kuwa muafaka umekubaliwa wa kuwaondoa watu waliojeruhiwa vibaya, kutoka katika ngome ya mwisho iliyokuwa ikishikiliwa na waasi katika mji wa Douma, huko Ghouta Mashariki.
Makubaliano hayo yanafuatia majadiliano ya kina yaliyohusisha kundi kuu la waasi la Jaish al-Islam, Urusi, pamoja na viongozi kadhaa wa kisiasa.
Kwa njia ya taarifa, Jenerali mmoja wa jeshi la Syria, amesema kwamba eneo zima la Ghouta Mashariki-- bila ya kuhusisha Douma -- kwa sasa, liko chini ya udhibiti wa jeshi la nchi hiyo.
Kufuatia majuma kadhaa ya milipuko ya mabomu, maelfu ya waasi waliamua kujisalimisha chini ya makubaliano ya kuwapa njia ya kukimbilia usalama wao, hadi maeneo ya Idlib- Kaskazini mwa Syria.
Jeshi la Rais Bashar Al Assad, sasa linasema kuwa waasi wachache waliosalia mjini Douma, pia wanafaa kuondoka mara moja, lau sivyo wakabiliwa na nguvu zote za kijeshi.
Jeshi la Urusi limekuwa likisimamia uhamisho huo wa waasi na familia zao kutoka Ghouta MasharikiHaki miliki ya pichaAFP
Image captionJeshi la Urusi limekuwa likisimamia uhamisho huo wa waasi na familia zao kutoka Ghouta Mashariki
Tunafahamu nini kuhusiana na muafaka huo?
Waasi huko Douma wamekanusha kuwa kupanga mashauriano ya kujiondoa kutoka ngome yao kwa pamoja na maelfu ya raia ambao wangali wakiishi huko.
Hata hivyo, waliojeruhiwa watakubaliwa kuondoka kwa hiari katika makubaliano hayo yaliyoafikiwa wanajeshi wa Urusi Jumamosi jioni.

No comments:

Post a Comment