TCU imeacha kuwapangia wanafunzi vyuo kutokana na agizo lililotolewa na Rais John Magufuli mwaka huu, alipozindua mabweni ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Ofisa Uhusiano wa Udom, Beatrice Baltazar amesema jana Jumanne Oktoba 31,2017 kuwa, katika mwaka wa masomo wa 2016/17 walipata wanafunzi 4,500 kutoka TCU.
Amesema mwaka huu wa masomo wamepata maombi ya wanafunzi 43,000 na waliochaguliwa ni 12,000 ambao wamekidhi vigezo.
Amesema ili kudhibiti tatizo la msongamano wa wanafunzi wanaosajiliwa chuoni hapo wameboresha utaratibu kwa kuongeza watumishi wanaowasajili na huduma za benki kusogezwa chuoni.
Ofisa huyo amesema Benki ya CRDB inatoa huduma kwa kutumia tawi linalohamishika na kuwa na mawakala, hivyo wanafunzi hufungua akaunti chuoni badala ya kwenda mjini.
Meneja wa Tawi la CRDB Udom, Chabu Mishwaro amesema wameamua kusogeza huduma karibu na wanafunzi ili kupunguza usumbufu ambao
wanaupata katika mchakato wa usajili.
Mwanafunzi aliyesajiliwa katika chuo hicho, Ikupa Mwambene amesema kusogezwa huduma kumemsaidia kutopata usumbufu wa kwenda kutafuta huduma na hatari ya kuibiwa na matapeli.
No comments:
Post a Comment