Monday, November 13

Trump asema ana ''uhusiano mzuri'' na Durtete

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa ana uhusiano mzuri na kiongozi wa Phillipino Rodrigo Durtete bada ya mkutano kati ya viongozi hao.
Image captionRais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa ana uhusiano mzuri na kiongozi wa Phillipino Rodrigo Durtete bada ya mkutano kati ya viongozi hao.
Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa ana uhusiano mzuri na kiongozi wa Phillipino Rodrigo Durtete bada ya mkutano kati ya viongozi hao.
Haijabainika iwapo Trump alizungumza kuhusu ukiukaji mkubwa wa haki za kibinaadamu nchini humo licha ya shinikizo za yeye kufanya hivyo.
Utawala wa Marekani uliopita ulimshutumu rais Durtete kuhusu vita vyake dhidi ya mihadarati ambavyo vimesababisha vifo vya watu 4000.
Bwana Trump anakaribia kukamilisha ziara yake ya bara Asia.
Mkutano wa kwanza kati ya Trump na Durtete ambao ulifanyika katika mkutano wa muungano wa mataifa ya kusini mashariki mwa bara Asia ASEAN ulitazamwa kwa makini kwa kuwa wote wawili wanajulikana kwa kutoa cheche kali za maneno zenye utata.
Baada ya mkutano huo wa faragha, rais huyo wa Marekani hakujibu maswali kuhusu iwapo alizungumzia kuhusu ukiukaji wa haki za kibinaadamu huku msemaji wa Durtete akisema kuwa hoja hiyo haikuzungumziwa.
Msemaji wa Ikulu ya Whitehouse Sarah Sanders baadaye alisema kuwa hoja hiyo ilijadiliwa kwa ufupi katika mkutano huo wa faragha hususan katika vita dhidi ya mihadarati lakini hakutoa maelezo zaidi.
Siku ya Ijumaa bwana Durtete alisema kuwa alimdunga mtu kisu hadi kufa wakati alipokuwa kijana.
Msemaji wake baadaye alisema kuwa matamshi hayo yalikuwa ya ndani.

No comments:

Post a Comment