Monday, November 13

Emirates yanunua ndege 40 kutoka Boeng kwa dola bilioni 15

Boeing 787Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionEmirates yanunua ndege 40 kutoka Boeng kwa dola bilioni 15
Boeng imeanzisha maonyesho yake ya ndege huko Dubai kwa kutangaa mauzo makubwa mapya katika maonyesho hayo ya siku tano.
Ilitangaza kuwa Shirika la ndege la UAE la Emirates limeagiza ndege 40 za Boeng 787 Dreamliners, katika mkataba wa thamani ya dola bilioni 15.
Mwenyeki wa shirika hilo Sheikh Ahmed bin Saeed al-Maktoum, amesema kuwa Boeng imechaguliwa badala ya Airbus A350.
Emirates Boeing 777Haki miliki ya pichaEMIRATES
Image captionEmirates yanunua ndege 40 kutoka Boeng kwa dola bilioni 15
Alikuwa ametarajiwa kutoa tangazo kubwa la kuagiza ndege za Airbus A380 superjumbo wakati wa mkutano wa waandishi wa habari.
Airbus inahitajia ndege zake za A380 kuagizwa zaidii zikiwa ndizo ndege kubwa zinazotumika kwa sasa.
Emirates ndilo shirika la ndege kubwa zaidi mashariki ya kati likiwa mnunuzi mkubwa zaid ya Boeng 777 na lina ndege 165 zinazohudumu likiwa tena limeagiza ndege 164.
Airbus A380Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAirbus ilizindua ndege yake mpya ya A380 mapema mwaka huu

No comments:

Post a Comment