Mwanajeshi mmoja wa Korea Kaskazini amepigwa risasi na kujeruhiwa na wanajeshi wenzake wakati akijaribu kuvuka kwenda Korea Kusini akipitia mpaka wenye ulinzi mali.
Hata hivyo mwanajeshi huyo alifanikiwa kuvuka mpaka na sasa anaendelea kupata nafuu.
Alipigwa risasi kwenye mkono wake na pia kwenye bega.
Mwanajeshi huyo alivukia katika kijiji cha Panmunjon, ambapo makubaliano ya kumaliza vita vya Korea yalisainiwa mwaka 1953.
- Marekani yaionya vikali Korea Kaskazini
- Ndege za kivita za Marekani zapaa Korea
- Uwezo wa kombora jipya la Korea Kaskazini
Karibu watu 30,000 raia wa Korea Kaskazini wamehamia Korea Kusini tangu wakati huo lakini wengi huvuka kupitia China
Si jambo la kawaida kwa mtu yeyote kuvuka mpaka unaotenganisha nchi hizo mbili.
Hiki ndicho kisa cha nne cha mwanajeshi wa Korea Kaskazini kuvuka kupitia eneo lenye ulinzi mkali.
Korea Kaskazini na Kusini wako kwenye mzozo mkubwa tangu vimalizike vita mwaka 1953 na hakuna makubaliano rasmi ya amani yaliyotiwa sahihi kati yao.
No comments:
Post a Comment