Wednesday, November 29

Mwanamfalme Miteb aachiliwa huru baada ya kulipa $1bn Saudia

Mwanamfalme Miteb aachiliwa huru baada ya kulipa $1bn SaudiaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMwanamfalme Miteb aachiliwa huru baada ya kulipa $1bn Saudia
Mwanamfalme wa Saudia Miteb bin Abdullah ameachiliwa huru zaidi ya wiki tatu baada ya kukamatwa kwa madai ya kuhusika na ufisadi , maafisa wanasema.
Mwanamfalme Miteb ambaye alionekana kuwa miongoni mwa warithi wa ufalme huo aliachiliwa huru baada ya kukubali kutoa faini ya dola bilioni moja.
Ni miongoni mwa wanasiaasa na wafanyibiashara 200 waliokamatwa nchini humo kutokana na vita dhidi ya ufisadi mnamo terehe 4 mwezi Novemba.
Watu wengine watatu pia wameachiliwa huru baada ya kukubali kulipa faini.
Ni kweli mwanamfalme Miteb aliachiliwa huru leo alfajiri {Jumanne} kulingana na duru zilizopo karibu na serikali zilizoambia chombo cha habari cha AFP.
Miteb ambaye ni binamu wa mwanamfalme Mohammed bin Salman na ambaye aliongoza kitengo cha walinzi wa kulinda ufalme huo ndiye aliyekuwa na ushawishi mkubwa zaidi wa kisiasa kukamatwa katika vita hivyo dhidi ya ufisadi.
Mwana huyo wa mfalme Abdullah alifutwa kazi muda mfupi kabla ya kuzuiliwa.
Wanawafalme, mawaziri na wafanyibiashara wakuu walikamatwa mwanzoni mwa mwezi huu na kuzuiliwa katika hoteli moja ya kifahari kwa madai ya ufisadi.

No comments:

Post a Comment