Kampuni ya Apple imesema kuwa inarekebisha tatizo kubwa katika mfumo wake wa operesheni wa Mac.
Tatizo hilo katika toleo lake jipya la MacOS High Sierra,l inaruhusu mtu yeyote kuingia katika mashine hiyo bila kutumia neno la siri na kupata haki zote za mtumizi wa mashine hiyo.
''Tunarekebisha programu ili kuliangazia swala hilo'', Apple ilisema katika taarifa.
Tatizo hilo lilifichuliwa na mtaalam wa maswala ya usalama wa mitandaoni nchini Uturuki Lemi Ergin.
Alifuchua kwamba kwa kutumia jina la mtumiaji ''root'' bila kujaza neno la siri na kubonyeza ''enter'' mara kadhaa atapata fursa kadhaa za kuingia katika kifaa hicho.
Hatahivyo bwana Ergin alikosolewa kwa kutofuata maelezo ya ufichuzi huo yanayofuatwa na wataalam wengine wa usalama wa mitandao.
Maelezo hayo yanawahitaji wataalam wa usalama wa mitandaoni kuelezea kampuni kuhusu mapungufu katika bidhaa zao hivyobasi kuwapatia muda wa kutosha kurekebisha tatizo hilo kabla ya kutangaza kwa umma.
Bwana Ergin hakutoa tamko lolote kuhusu madai hayo wakati alipoulizwa katika mtandao wa Twitter na BBC ilishindwa kumpata siku ya Jumanne.
Apple haikuthibitisha wala kukataa iwapo iligundua tatizo hilo mapema .
No comments:
Post a Comment