Idadi hiyo imepungua ikilinganishwa na takwimu za mwaka 2015 zinazoonyesha kuwa idadi ya watoto waliokuwa wakipoteza maisha yao kila siku ilikuwa 2015.
Akizungumza katika Mafunzo ya namna ya kuandika habari za watoto yanayoendeshwa na Jukwaa la Wahariri nchini (TEF), Mtaalamu wa masuala ya kuzuia maambukizo ya Vrusi vya Ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa Mtoto kutoka Shirika la Afya Duniani (Unicef), Hafsa Khalfani amesema malaria na magonjwa yatokanayo na lishe duni yanachangia vifo hivyo.
Khalfani amesema asilimia 34 ya watoto nchini wana utapiamlo, 20 hawapati mlo kamili, 40 hawapati haki zao za msingi wakati asilimia 75 wameshafanyiwa ukatili.
Mtaalamu huyo amesema huyo changamoto zinazowahusu watoto zinaweza kutatuliwa ikiwa kila mmoja ikiwamo waandishi wa habari watashiriki kuzitatua.
Mwenyekiti wa TEF, Theophil Makunga amesema mafunzo hayo yanafanyika ili kuwanoa waandishi kuhusu habari za watoto kutokana na umuhimu wa kuwapo kwaajili ya kuandika kiweledi habari za watoto lazima waandishi wa habari wabobee kwenye eneo hilo.
Katika hatua nyingine, Ofisa Habari wa Unicef, Usia Nkoma amesema wazazi wana jukumu la kuhakikisha watoto wao wanasafiri kwenye shule na kurejea nyumbani kwenye usalama.
Amesema wazazi na walezi wamekumbushwa wajibu wao wa kuwalinda watoto baada ya baadhi ya tafiti kuonyesha moja ya maeneo wanayofanyiwa ukatili wa ngono kwenye mabasi ya shule.
Nkoma amesema mtoto wa kwanza kuingia kwenye gari la shule na wa mwisho kushuka wapo hatarini kufanyiwa ukatili huo, ikiwa usafiri huo utabaki na watumishi bila usimamizi wa walimu au walezi.
“Hata kama mzazi umebanwa na kazi bado jukumu la kuhakikisha mtoto yupo salama, mfano tu kwenye masuala ya usafiri mtoto wa kwanza kuingia kwenye basi la shule na wa mwisho, ikiwa basi hilo halina muhudumu mwingine au mwalimu ni hatari kwa hiyo, wanafanyiwa ukatili wa kingono,” amesema ma.
Makunga amesema waandishi wa habari wanalo jukumu la kuandika habari zinazowahusu watoto ili kuendelea kuikumbusha jamii itimize wajibu wao.
Akifundisha masuala ya sheria za watoto, Jesse Kwayu amesema chanzo kikubwa cha uhalifu ni malezi hafifu ya watoto.
“Hivi mmewahi kujiuliza mtoto wa mtaani anapokua mtu mzima anaenda wapi? Jambo hili kila mmoja anapaswa kutafakari kwa sababu vinginevyo kila mmoja ataathirika na hili,” amesema.
No comments:
Post a Comment