
Kimbunga kwa jina Damrey ambacho kimekuwa kikipiga maeneo ya kusini na kati ya Vietnam kimesababisha vifo vya watu 27, na wengine zaidi ya 20 hawajulikani waliko.
Kimbunga hicho kilifika maeneo ya bara Jumamosi kikiwa na upepo unaovuma kwa kasi ya kilomita 90 kwa saa.
Nyumba zaidi ya 40,000 zimeharibiwa vibaya na maelfu ya watu wamehamishwa makwao.
Maeneo mengi pia hayana umeme.
Eneo lililoathiriwa zaidi ni jiji la Nha Trang - umbali wa 500km hivi kusini mwa jiji la Da Nang katika pwani ya nchi hiyo ambapo viongozi wa mataifa wanachama wa Apec (Jumuiya ya Kiuchumi ya Asia na Pasific) wanatarajiwa kuhudhuria mkutano mkuu baadaye wiki hii.







No comments:
Post a Comment