Rais wa Marekani Donald Trump, amesema kwamba Japan itatungusha makombora ya Korea Kaskazini "kuziondoa angani" kwa kutumia mitambo ya kijeshi yaliyonunuliwa kutoka Marekani.
Wakati huo huo, waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe, amesema kwamba, taifa lake litadungua makombora hayo kabla ya kutua ardhini, "ikiwa hilo litahitajika".
Viongozi hao wawili, walisema hayo walipozungumza na waandishi habari wakati wa kumalizika rasmi kwa ziara ya kwanza ya kitaifa ya Bwana Trump nchini Japan.
Katika miezi ya hivi karibuni, Korea Kaskazini imerusha makombora mawili hatari juu ya mipaka ya Japan.
Trump aapa kukabiliana na Korea Kaskazini kwenye ziara yake ya Bara Asia.
Alipokuwa akijibu maswali ya waandishi habari leo Jumatatu, Bw Trump alisema kwamba, Bwana Abe atanunua "kiasi kikubwa cha zana za kivita" kutoka Marekani.
Akigusia zana hatari za kinuklea za Korea Kaskazini, Trump alisema kuwa Bw Abe "atazishambulia zikiwa bado angani" mara tu atakapokuwa amemaliza kununua silaha hizo za kijeshi, anazosema kuwa itatoa ajira ya kazi kwa Wamarekani na pia "kutoa usalama kwa Japan".
No comments:
Post a Comment