Chatu mkubwa alikumbana na kifo kibaya baada kwa kuuliwa, alilipopoteza vita vikali kwa mwanamume mmoja nchini Indonesia.
Mlinzi Robert Nababanm, alikumbana na chatu huyo kwenye shamba moja la michikichi wilaya ya Batang Gansal huko Sumatra Indonesia.
Bw Nababan akajaribu kumshika chatu huyo ambaye anaripotiwa kuwa wa urefu wa mita 7.8.
- Mwanamume aliyetoweka apatikana ndani ya chatu Indonesia
- Jinsi magari yasiyo na dereva hukanganywa na kangaroo.
Chatu huyo alimshambulia na wote hao wakamenyana hadi pale Bw. Nababan alipomuua chatu huyo akisaidiwa na wanakijiji.
Mlinzi huyo alinusurika na majeraha mabaya.
Hata hivyo chatu huyo hakubahati vile Bw. Nababan alivyobahatika, aliwekwa kwenye maonyesho kijijini, kabla ya kukatwa katwa, akakaangwa na kuliwa.
Nababan 37, hakusema sababu iliyochangia amshike chatu huyo lakini alisema kuwa kulikuwa na wanavijiji ambao hawangevuka barabara kwa sababu ya chatu huyo.
Ripoti zinazokinzana zinasema kuwa labda alitaka kuwahakikishia usalama wanavijiji au alitaka kumuondoa chatu huyo barabarani.
Polisi waliliambia shirika la AFP kuwa chatu huyo alikuwa amemeza mkono wake na nusura autafune.
Alipelekwa hospitalini katika mji wa Pekanbaru ambapo anaendelea kupata nafuu lakini mkono wake huenda ukakatwe.
Kisa kingine cha mwezi machi kilishia vibaya wakati mwanamume nchini Indonesia alipatika amekufa ndani ya tumbo la chatu.
No comments:
Post a Comment