Thursday, October 5

Hispania yakataa wito wa Catalonia

Kushoto ni kiongozi wa Catalonia na kulia ni Mfalme FelipeHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionKushoto ni kiongozi wa Catalonia na kulia ni Mfalme Felipe
Serikali ya Hispania imeukataa wito uliotolewa na kiongozi wa Catalonia, Carles Puigdemont kuwepo kwa mapatano juu ya matakwa ya uhuru wa jimbo hilo.
Ofisi ya Waziri mkuu Mariano Rajoy, imesema Madrid haitokubali kusalitiwa na hivyo hakutakuwa na mazungumzo mpaka pale kiongozi huyo wa Catalonia atakapoachana na madai yake ya kampeni zisizo halali za kudai uhuru.
Awali Carles Puigdemont aliikosoa hotuba aliyoitoa Mfalme Felipe wa Hispania, ambaye aliiita kura ya maoni juu ya uhuru wa jimbo hilo, iliyofanyika siku ya Jumapili kuwa ni tendo lisilo ruhusiwa la kisaliti.
Mgogoro huo wa Catalonia umepiga soko la Hisa la Hispania siku ya Jumatano na kuonekana anguko lake la siku katika kipindi cha miezi 15.
Wakazi wa CataloniaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWakazi wa Catalonia
Serikali ya Catalonia imesema kutakuwa na kikao maalumu cha bunge siku ya Jumatatu kuzungumzia matokeo ya zoezi la kura hiyo ya maoni, lililokumbwa na mgawanyiko.
Licha ya maafisa wa Catalonia kusema kwa kura hiyo ya maoni iliungwa mkono kwa asilimia 90, matokeo rasmi bado hayajatangazwa.
Kura hiyo imekadiriwa kuungwa mkono kwa asilimi 42.
katika taaifa yake ta siku ya Jumatatu, Bw Puigdemont hakufafanua zaidi juu ya uwezekano wa kutangaza uhuru.
Akitumia lugha ya Catalonia aliwashukuru raia wa Hispania ambao walionyesha uzalendo wao kwa Catalonia.

No comments:

Post a Comment