Thursday, October 5

Mabaki ya meli ya abiria Athenia iliyozamishwa 1939 yagunduliwa baharini

SonarHaki miliki ya pichaGSI
Image captionMabaki yanayoaminika kuwa ya Athenia
Mabaki ya meli ya kwanza kuzamishwa wakati wa vita vya pili vya dunia yanaonekana kupatikana katika sakafu ya bahari ya Atlantic.
Mwindaji wa mabaki ya meli David Mearns, anasema inaonekana kuwa mabaki meli hiyo ya abiria ya Athenia huenda yapo mita 200 chini ya bahari nje ya pwani ya Ireland.
Nyambizi ya Ujerumani iliizamisha meli hiyo saa kadhaa baada ya Uingereza kutangaza vita dhidi ya Hitler mwaka 1939 ambapo zaidi ya watu 100 wengi raia wa Marekani waliuawa.
Illustration of Athenia
Image captionAsilimia kubwa ya abiria walikuwa ni wanawake na watoto
Ujerumani ilikana kuhusika kutokaka na hofu kuwa Marekani ingejiunga kwenye vita hivuo.
Kamanda wa nyambizi ya Ujerumani alikuwa amedhania kimakosa kuwa meli hiyo ya abiria ilikuwa ni manowari ya kivita.
Hata wakajaribu kumzingizia Winston Churchill, ambaye siku hiyo alikuwa ameteuliwa kamanda wa jeshi la Uingereza.
Ujerumani ilisema kuwa alikuwa ameamrisha nyambizi ya Uingereza kuishambulia Athenia kama sehemu ya njama ya kuilazimisha Marekani kujiunga kwenye vita.
Ukweli kamili ulibainika wakati wa kesi za Neremberg.
Athenia
Image captionAthenia

No comments:

Post a Comment