Thursday, October 5

Mama afungwa siku 7 kwa kukataa kuruhusu mtoto kupewa chanjo Marekani

Rebecca BredowHaki miliki ya pichaWXYZ
Image captionRebecca Bredow alikataa kutekeleza agizo la mahakama la kumruhusu mtoto apate chanjo
Mama wa mtoto katika jimbo la Michigan nchini Marekani amehukumiwa kifungo cha siku 7 jela baada ya kukataa agizo la jaji la kutaka ampeleke mtoto wake kupewa chanjo.
Rebecca Bredow hakuruhusu mtoto wake wa kiume wa umri wa miaka 9 apate chanjo baada ya kukubaliana awali na baba ya mtoto afanye hivyo.
Mumewe wa zamani kwa sasa amepewa ruhusa ya kumtunza mtoto huyo kwa muda ili aweze kupata chanjo.
Rebecca BredowHaki miliki ya pichaCOURT
Image captionRebecca Bredow hakuruhusu mtoto wake wa kiume wa umri wa miaka 9 apate chanjo baada ya kukubaliana awali na baba ya mtoto afanye hivyo.
Wazazi katika jimbo la Michigan wanaruhusiwa kisheria kukosa au kuchelewesha kuchanjwa watoto wao kutokana na imani zao.
Lakini Bredow alikiuka sheria hiyo kwa sababu alikataa kutimiza makubaliano na mume wake wa zamani ya Novemba mwaka 2016 ya kuruhusu mtoto huyo apewe chanjo.
Mama huyo wa watoto 2 alihukumiwa siku ya Jumatano kwa kupuuza amri ya mahakana ya wiki iliyopita ya kumtaka amruhusu mtoto wake apewe chanjo.

No comments:

Post a Comment