Mfalme Salman wa Saudi Arabia amewasili Moscow, ikiwa ni ziara ya kwanza kwa mtawala wa kifalme wa nchi hiyo kutembelea Urusi.
Katika ziara yake hiyo, atafanya mazungumzo na mwenyeji wake, Rais Vladmir Putin, ikiwa ni dalili ya jinsi uhusiano wao ulivyo karibu katika siku za karibuni.
Majadiliano kati ya mataifa hayo mawili yanayoongoza duniani kwa usafirishaji wa mafuta yanatarajiwa kulenga katika ushirikiano katika uzalishaji wa mafuta pamoja na kusaini mikataba kadhaa ya uwekezaji.
Mustakabali wa Syria, nchi ambayo Saudia na Urusi zimekuwa zikiunga mkono pande tofauti katika vita vinavyoendelea, pia utazungumziwa
No comments:
Post a Comment