Thursday, October 5

Wanajeshi 3 wa Marekani wameuawa nchini Niger

Map of Niger
Image captionWanajeshi 3 wa Marekani wameuawa nchini Niger
Wanajeshi wa watatu wa Marekani wameuawa na wengine wawili kujeruhiwa baada ya kuviziwa nchini Niger karibu na mpaka na Mali.
Wanajeshi kadha wa Niger nao pia wanaripotiwa kuuliwa kwenye shambulizi hilo.
Wanajeshi hao walishambuliwa vikali walipokuwa wakipiga doria.
Jeshi la Marekani limekuwa likitoa mafunzo kwa jeshi la Niger linalopambana na wanamgambo wa kiislamu eno hilo, na dhidi ya tawi la kundi la al-Qaeda kaskazini mwa Afrika.
Rais wa Marekani Donald Trump amejulishwa na mkuu wake wa majeshi John Kelly kuhusu shambulio hilo, kwa mujbu wa msemaji wa Ikulu ya White House, Sarah Sanders.
Kwa mujibu na New York Times makomando watatu wa Marekani waliuawa kwenye uvamizi huo uliotokea kilomita 193 kutoka mji mkuu wa Niger Niamey.
Gazeti hilo lilisema hao ndio wanajeshi wa kwanza wa Marekani kuuliwa kwa kuviziwa tangu kikosi hicho cha Marekani kitumwe kwenda Niger.
Afisa kutoka eneo la Tillaberi nchini Niger aliliambia shirika la Reuters kuwa wanajeshi 5 wa Niger ni miongoni mwa wale waliouawa.

No comments:

Post a Comment