Wizara ya ulinzi nchini Afghanistan imesema mlipuko mmoja wa mjitoa mhanga Jumamosi nje ya shule ya utoaji mafunzo ya kijeshi mjini Kabul uliuwa wanafunzi wasiopungua 15 na kuwajeruhi wengine kadhaa.
Shambulizi hilo limetokea siku moja baada ya mjitoa mhanga mmoja wa kundi la Islamic State-IS kushambulia msikiti uliojaa waislam wa dhehebu la kishia katika mji huo na kuuwa waumini 50 na kuwajeruhi darzeni wengine.
Polisi wa Afghanistan pamoja na mashahidi walisema shambulizi la Jumamosi lilitokea baada ya mjitoa mhanga aliyekuwa akitembea kwa miguu kujilipua karibu na basi dogo lililojaa wanafunzi wa jeshi kwenye mlango mkuu wa kuingilia kwenda shule ya utoaji mafunzo ya jeshi ya Marshal Fahim. Msemaji wa wizara ya ulinzi Dawlat Waziri alithibitisha idadi ya vifo na alisema watu wane wengine walijeruhiwa.
No comments:
Post a Comment