Adhanom Ghebreyesus, amesema kuwa anafikiria upya, uamuzi wake wa kumteuwa Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, kuwa balozi wa nia njema wa shirika hilo kubwa la Afya Duniani.
Hii inafuatia ukosoaji mkubwa kutoka kwa viongozi mbalimbali ulimwenguni, kutokana na uamuzi huo wa kumteuwa Mugabe ambaye anayelaaniwa na watu wengi duniani.
Sasa Ghebreyesus, amesema kuwa atatoa taarifa mpya hivi karibuni kuhusiana na uamuzi huo.
Serikali ya Uingereza inasema, imeshtushwa na kuvunjika moyo, kuwa shirika la Afya Duniani, WHO, limemtaja rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, kuwa balozi wa nia njema.
Msemaji mjini London, alieleza kuwa bwana Mugabe anakabili vikwazo vya Marekani na Umoja wa Ulaya, na kuteuliwa kwake, kutaathiri kazi za WHO.
Akifafanua uamuzi wa uteuzi huo , Mkurugenzi mkuu mpya wa W.H.O, Dr Tedros Adhanom Ghebreyesus, alisifu namna Zimbabwe inavyozingatia afya ya umma.
Lakini wakosoaji wanasema katika kipindi cha miaka thelathini na saba ya utawala wa rais Mugabe, huduma za afya zimekuwa mbaya ambapo wahudumu wa afya wamekuwa hawalipwi mara kwa mara , na kumekuwa na ukosefu mkubwa wa dawa muhimu .
Dr .Tedros, ni raia wa Ethiopia ambaye ni Muafrika wa kwanza kuongoza shirika la W.H.O. na alichaguliwa kwa ajili ya kukabiliana na kile kilichoaminiwa kuwa ni kugeuzwa kwa shirika hilo kuwa la kisiasa.
No comments:
Post a Comment