Sunday, October 22

Nchi imekosa mapatano, haina shabaha moja dhidi ya maadui



Nairobi, Kenya. Umoja wa Mataifa (UN) umesitisha shughuli zake zote nchini Kenya katika kipindi cha kuelekea uchaguzi wa marudio wa Oktoba 26.
Taarifa iliyotolewa Ijumaa na Msaidizi wa Katibu mkuu kanda ya Afrika Mashariki, Peter Drennan imesema umoja huo utasitisha kwa muda programu zake zote ambazo hazikuwa muhimu sana.
“Baada ya kufanya tathmini ya hali ya usalama nchini Kenya, ofisa mteule (DO) kwa ushauri kutoka Timu ya Usimamizi wa Usalama, ameshauri kusitishwa kwa warsha, mikutano, semina na makongamano na jumbe mbalimbali zisizo za lazima nchini Kenya walau kwa wiki moja kabla na wiki moja baada ya uchaguzi wa marudio kwa kura ya urais,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.
“Ninakubaliana na ushauri wa DO na mamlaka husika kusitishwa kwa programu hizo ambazo hazina ulazima kuanzia leo Oktoba 19 hadi Novemba 2.”
Jana Alhamisi serikali ilitangaza kwamba Alhamisi ya Oktoba 26 itakuwa siku ya mapumziko kwa ajili ya kuruhusu wananchi kushiriki uchaguzi wa marudio.
Kaimu Waziri wa Mambo ya Ndani, Fred Matiang’i alitangaza kwamba siku hiyo imeandikwa katika Gazeti la Serikali kwamba itakuwa siku ya mapumziko kuwezesha Wakenya kushiriki kwa uhuru uchaguzi huo.
Tangazo hilo limekuja katikati ya mnyukano wa kisiasa na kuiweka uchaguzi huo katika hatihati ya kufanyika.
Jumatano, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Wafula Chebukati alielezea kukerwa kwake katika maandalizi ya uchaguzi wa marudio na akatangaza wazi kuwa hawezi kuhakikisha uchaguzi wa kuaminika.
Chekubati alisema kutokana na kupanda sana kwa hofu ya kisiasa nchini, alipendekeza Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga wakutane kwa mazungumzo kabla ya uchaguzi huo.

No comments:

Post a Comment