Tuesday, October 10

Ufaransa yaelezea operesheni za wahamiaji wa Niger na Chad

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anasema kwamba operesheni ya kwanza ya kuruhusu wahamiaji kuingia kihalali nchini Ufaransa kutoka nchini Niger na Chad itaanza katika wiki chache zijazo.
Rais Macron alisema operesheni ijayo itaongozwa na ofisi ya kulinda wakimbizi ya Ufaransa kufuatia mkutano wa Jumatatu na kamishna mkuu kwa masuala ya wakimbizi wa Umoja wa Mataifa, Filippo Grandi huko ikulu ya Elyzee.
Katika mkutano wa Paris mwezi Agosti viongozi wa Ufaransa, Ujerumani, Italy na Spain walikubaliana kufanya operesheni ya usalama katika mataifa hayo ya Afrika kwa kushirikiana na idara za wakimbizi na wahamiaji za Umoja wa Mataifa. Utaratibu utawaruhusu wahamiaji waliyo hatarini kupatiwa hifadhi ya kisiasa na kuingia kihalali ulaya kama wapo kwenye orodha halali iliyowasilishwa na idara ya wakimbizi katika Umoja wa Mataifa na kusajiliwa na maafisa huko Niger na Chad.

No comments:

Post a Comment