Tuesday, October 10

Sheriff wa Nevada anakerwa na uchunguzi unavyofanywa taratibu Las Vegas

Sheriff Joe Lombardo
Zaidi ya wiki moja baada ya mtu mwenye bunduki Stephen Paddock alipouwa watu 58 na kuwajeruhi zaidi ya watu 500 wengine wachunguzi huko Las Vegas katika jimbo la Nevada bado hawajafahamu kilichochochea ufyatuaji mbaya wa risasi wa umma katika historia ya Marekani.
Sheriff wa Nevada katika wilaya ya Clack, Joe Lombardo alisema Jumatatu kwamba ana kerwa na jinsi uchunguzi unavyofanyika pole pole akisema Paddock kwa makusudi alificha vitendo vyake kabla ya kufanyika uhalifu huu.
Wachunguzi wakiwa juu ya jengo la tukio
Wachunguzi wakiwa juu ya jengo la tukio
Lombardo alisema “hakuna ushahidi hadi wakati huu unaoonesha kwamba kulikuwa na mfyatuaji risasi wa pili, hakuna ishara Lombardo aliyoona kwa mtu mwingine yeyote huko Las Vegas na hakuna uhusiano wa makundi ya ugaidi au itikadi nyingine yeyote”. Sherif pia alisema wachunguzi hawaamini kwamba tukio moja lilimshinikiza Paddock kufanya kile alichokifanya.
Sheriff huyo pia alitangaza mabadiliko muhimu katika kipindi cha Oktoba mosi. Aliwaambia waandishi wa habari Jumatatu kwamba Paddock alimfyatulia risasi mlinzi wa usalama kwenye hoteli ya Mandalay Bay dakika sita kabla ya kuanza kufyatua risasi kwenye mkusanyiko unaoangalia tamasha la muziki wa Country.

No comments:

Post a Comment