Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe siku ya Jumatatu alimhamisha Patrick Chinamasa kutoka wizara ya fedha kwenda kuongoza wizara mpya ya usalama wa mtandao ambayo italenga juu ya uhalifu wa mitandao ya kijamii na tovuti nyingine kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka ujao.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters nafasi ya Chinamasa inachukuliwa na waziri wa mambo ya ndani Ignatius Chombo katika mabadiliko ya baraza la mawaziri ambapo pia linapunguza jukumu la Makamu Rais Emmerson Mnangagwa anayeonekana atachukua nafasi ya Rais Mugabe.
Mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri yalitangazwa katika taarifa ya serikali iliyotolewa wakati kuna upungufu mkubwa sana wa sarafu ambao ni pigo jipya kwa uaminifu na uwekezaji katika uchumi wa taifa hilo la kusini mwa Afrika ambalo linatumia dola ya Marekani.
No comments:
Post a Comment