Saturday, October 28

Teodorin Obiang: Makamu wa rais wa Equatorial Guinea ahukumiwa kufungwa jela Ufaransa

ObiangHaki miliki ya pichaAFP
Mahakama moja nchini Ufaransa imemhukumu makamu wa rais wa Equatorial Guinea Teodorin Obiang kifungo cha miaka mitatu jela ambacho kimeahirishwa.
Bw Obiang, 48, hufahamika sana kutokana na maisha yake ya anasa.
Ni mwanawe rais wa taifa hilo la Afrika Magharibi.
Hakuwepo mahakamani wakati mahakama ilipomkuta na hatua ya ubadhirifu wa mali ya umma.
Mali yake Ufaransa itatwaliwa, ikiwa ni pamoja na jumba la kifahari eneo la Avenue Foch jijini Paris. Kadhalika amepigwa faini ya euro 30m (£27m; $35m) ambayo imeahirishwa.
Obiang alikuwa ameshtakiwa kwa kutumia fedha za serikali kufadhili maisha ya anasa katika mji mkuu wa Ufaransa Paris.
Miongoni mwa mali aliyotumia fedha hizo kununua, ni pamoja na majengo ya kifahari yenye kugharimu zaidi ya dola milioni 100, boti la kifahari lenye urefu wa mita 76, na magari mengi ya kifahari kama vile Bugatti, Ferrari na Rolls Royces.
Waendesha mashtaka nchini Marekani tayari walikuwa wamemlazimisha kupeana mali kadhaa likiwemo jumba lenye thamani ya milioni 30 huko California na katika maskani ya Michael Jackson.
Babake Teodoro Obiang Nguema, amekuwa mamlakani tangu mwaka 1979 na ndiye rais wa Afrika aliyetawala kwa muda mrefu zaidi.

No comments:

Post a Comment