Mabaharia wawili raia wa Marekani na mbwa wao wawili wameokolewa na jeshi la wanamaji la Marekani karibu miezi mitano chombo chao kikielea katika bahari ya Pacific kwa mujibu wa maafisa.
Jennifer Appel na Tasha Fuiaba walianzia safari yao huko Hawaii wakielekea Tahiti wakati injini ya mashua yao ilikumbwa na hitilafu kutokana na hali mbaya ya hewa.
Mashua yao kisha ikaendelea kuelea baharini katika umbali wa kilomita 1,500 kusini mashariki mwa Japan.
Waliokolewa baada ya meli za uvuzi kuujulisha utawala wa Marekani.
Wanawake hao walianza safari yao mwezi Mei na walifikiri kuwa wangefika ardhini wakielea kwa nguvu za upepo, jeshi la wanamaji la Marekani lilisema katika taarifa.
Miezi miwili baada ya kuanza safari yao na muda ambao walikuwa wamekadiria wangekuwa wamefika Tahiti, walianza kutuma ishara za kuomba msaada.
Jeshi la Marekani linasema kuwa wanakake hao waliendelea kutuma ishara za kila siku lakini ishara hizo hazikuoneka kwa sababu walikuwa mbali na vyombo vingine vya majini au karibu na vituo viivyo ardhini.
Lakini Oktoba 24, meli ya uvuvi ya Taiwan ilitambua mashua hiyo baharini na kuzijulisha mamlaka za Marekani katika kisiwa cha Guam.
Meli ya USS Ashland ambayo ilikuwa eneo hilo iliwasili kesho yake kuwakoa mabaharia hao kutoka Honolulu pamoja na mbwa wao.
No comments:
Post a Comment