Mwanamuziki nyota wa Afrobeats nchini Uganda, ambaye sasa amekuwa mbunge Bobi Wine, ni mwanasiasa wa hivi punde kurejesha dola 8,000 ambazo ni pesa zilizotolewa kwa wabunge.
Wabunge wote 429 walipewa pesa hizo kuwasaidia kuongea na sehemu zao za uwakilishi kuhusu kipengee chenye utata kuhusu umri wa kuwania urais.
Mswada huo ni hatua ya chama tawala cha NRM kuondoa umri wa kuwania urais ambao kwa sasa ni miaka 75.
Inaonekana kuwa sehemu ya mpango ya kumwezesha Rais Yoweri Museveni, 73, kuwania muhula wa sita mwaka 2021.
Wine aliandika katika mtandao wa Facebook kuwa alikuwa ameishauri benki yake kurudisha fedha hizo kwa yule aliyezituma.
Alisema kuwa ni jambo la kusikitisha kuwa pesa hizo zilikuwa zikipeanwa kwa wabunge wakati waendesha mashtaka, maafisa wa mahakama, madaktari , walimu na maafisa wengine wa serikali wako kwenye migomo au wanataka kugoma kutokana na mazingira mabaya ya kazi.
No comments:
Post a Comment