Hivi karibuni akiwa wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro kuzindua mradi wa kusambaza umeme vijijini awamu ya tatu kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Dk Kalemani aliwaagiza mameneja wa mikoa wa Tanesco kuanzisha madawati ya huduma kwa wateja katika ofisi zote za wilaya na mikoa nchini.
Katika kutekeleza agizo hilo, Meneja Mwandamizi wa Tanesco Kanda ya Kaskazini, Mhandisi Stela Hiza ameongoza timu ya watumishi wa shirika hilo mkoa kufungua ofisi ndogo tatu katika wilaya za Same na Mwanga.
Hiza amesema kutokana na adha iliyokuwa ikiwakabili wateja ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hiyo, shirika limewasogezea ofisi karibu.
“Tumelenga kufungua ofisi ndogo tisa katika maeneo ya wilaya za Mkoa wa Kilimanjaro, tumeanza na tatu katika Kata za Hedaru, Kisiwani na Spillway iliyopo Nyumba ya Mungu wilayani Mwanga,” amesema.
Amesema katika vituo hivyo vitatu, wanatarajia kutoa huduma kwa wakazi zaidi ya 18,000.
No comments:
Post a Comment