Kamishna wa Shirika la Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa ametoa maoni juu ya mgogoro ya kisiasa na usalama katika eneo wanaloishi watu wanaozungumza Kiingereza.
Katika taarifa iliyotolewa mwishoni mwa wiki iliyopita, shirika hilo la haki za binadamu limesema kuwa linawasiwasi na hatua kali iliyochukuliwa na serikali dhidi ya watu walioandamana kwa amani. Shirika hilo pia limeomba ufanyike uchunguzi huru ili kubaini udhibiti huo ulivyosababisha vifo.
“Tunaomba mamlaka ihakikishe kuwa vikosi vya usalama vinajizuia na vinachukua hatua za makusudi kuzuia matumizi ya nguvu wakati wanalinda maandamano,” ilisema taarifa hiyo.
“Watu wanapaswa kutumia haki ya kufanya mikutano ya amani na kuwa na uhuru wa kujieleza, ikiwa ni pamoja na kutokukatazwa kutumia mawasiliani ya mitandao.”
Shirika hilo limerudia wito uliotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ambaye wiki iliyopita aliwasihi kupunguza nguvu za kukabiliana katika maeneo ya Kaskazini Magharibi na Kusini Magharibi, amabako wananchi wanapigania uhuru wao kutoka kwa wenzao wanaozungumza Kifaransa nchini humo.
“Tunaitaka Serikali na makundi ya wanaharakati wanaozungumza Kiingereza kuanzisha mazungumzo ya kisiasa ili manung’uniko ya wanaozungumza Kiingereza, ambayo kimsingi ni ya miongo kadhaa, yanaweza kujadiliwa kikamilifu na kupatiwa ufumbuzi,” imesema taarifa hiyo.
Ingawa wanaopigania kujitenga wanasukuma ajenda yao hiyo wakiegemea upande wa Ambazonia, serikali kuu imesisitiza kwamba umoja wa nchi hiyo iliyoko Afrika ya Kati utabaki hivyo bila kuhojiwa wala majadiliano.
No comments:
Post a Comment