Lulu anajitetea katika kesi ya kuua bila kukusudia ya msanii mwenzake wa filamu marehemu Kanumba.
Akijitetea mahakamani leo Jumatatu, Lulu amesema Kanumba alikuwa akilewa ananipiga sana.
Amesema Kanumba alimpiga kwa panga mapajani na alipelekwa Hospital ya Mwananyamala.
“Sijasababisha kifo cha Kanumba kwa namna yoyote ile. Umbo langu na umbile langu lilikuwa dogo hivyo mimi ndiyo nilikuwa nashambuliwa,” amesema Lulu
“Kama marehemu asingeanguka labda angenidhuru. Kanumba alikuwa kama mlezi wangu tulianza mahusiano miezi minne kabla ya kifo chake.”
No comments:
Post a Comment