Monday, October 23

Catalonia: Maafisa wa jimbo kukaidi amri ya Uhispania

Catalan EsteladaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMaandamano ya kuunga mkono uhuru yalifanyika Barcelona siku ya Jumamosi
Viongozi wa jimbo la Catalania linalotaka kujitenga kutoka kwa Uhispania wamesema hawatafuata amri ya serikali kuu ya Uhispania iwapo serikali hiyo itachukua hatua za kulidhibiti jimbo hilo.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Catalonia Raul Romeva ameambia BBC kwamba serikali hiyo kuu inachukua hatua dhidi ya nia ya raia wa Catalonia.
Waziri Mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy ametangaza mpango wa kuivunja serikali ya jimbo hilo na kupunguza baadhi ya uhuru ambao umekuwa ukijivuniwa na bunge la jimbo hilo.
Vyama vinavyounga mkono uhuru wa Catalonia vitakutana baadaye leo kujadili hatua za kuchukua.
Bunge la Seneti la Uhispania linatarajiwa kuidhinisha mikakati ya serikali hiyo Ijumaa pamoja na pendekezo la kufanyika kwa uchaguzi mpya katika jimbo la Catalonia.
Tulifikaje hapa?
Serikali ya Catalonia, ikiongozwa na Rais Carles Puigdemont, imekataa kusitisha juhudi zake za kutaka kujitangazia uhuru kutoka kwa Uhispania baada ya kuandaa kura ya maoni iliyokuwa imeharamishwa na mahakama nchini humo mapema mwezi huu.
Jumamosi, Bw Rajoy alisema atatumia Kifungu 155 cha katiba - katika hatua isiyo ya kawaida - ambacho kinairuhusu serikali kuu kutekeleza udhibiti kamili wa moja kwa moja dhidi mojawapo kati ya majimbo yaliyo na mamlaka ya kujitawala katika nchi hiyo iwapo kutakuwa na mzozo.
Lakini viongozi wa Catalonia wamesema hawataukubali mpango huo.
Catalonia
Bw Romeva ameambia BBC Radio 4 kwamba: "Inawezekanaje Umoja wa Ulaya ukubali jambo kama hilo [iwapo litatokea]. Demokrasia ya EU inawezaje kuendelea kuwepo na wanawezaje kuaminika iwapo watakubali hili litokee?
"Kwa sababu ninaloweza kuwaambia ni kwamba watu na taasisi za Catalonia hawataruhusu haya yatokee," na kuongeza kwamba serikali ya Uhispania inatakiwa kutambua kwamba wakazi wa eneo hilo walipiga kura kujitenga.
Serikali ya Catalonia imesema kwamba kati ya 43% ya waliopiga kura wakati wa kura ya maoni tarehe 1 Oktoba, 90% waliunga mkono kujitenga.
Vyama vya kuunga mkono kusalia pamoja na Uhispania ambavyo vilipata 40% ya kura wakati wa uchaguzi wa jimbo la Catalonia mwaka 2015 vilisusia kura hiyo ya maoni, sawa na wakazi wengi wanaopinga uhuru wa Catalonia.
A woman walks past pieces of Catalan pro-independence graffiti on some doors in BarcelonaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Nini kitafuata?
Bw Puigdemont amesema serikali yake haitakubali kutawaliwa na Uhispania.
Kando na kumpokonya Carles Puigdemont mamlaka yake yote, serikali kuu inapanga pia kutaribu kutwaa udhibiti wa polisi wa Catalonia pamoja na runinga ya serikali ya jimbo hilo, TV3.

No comments:

Post a Comment