Moto katika msitu huko kaskazini mwa jimbo la California nchini Marekani uliendelea kusamba usiku wa Jumatano kutokana na upepo mkali na kulazimisha watu wengine kuhamishwa.
Moto unawaka kupitia karibu eneo lenye ukubwa wa heka 69,000 kwenye wilaya kadhaa maarufu duniani kwa utengenezaji wa mvinyo. Moto huo umeuwa watu 21 tangu Jumapili na zaidi ya watu 300 waliripotiwa kupotea. Lakini maafisa wanaamini watu wengi waliopotea bado hawajawasiliana na marafiki au familia zao.
Kiasi cha nyumba na biashara 3,500 zimeungua kwa kuteketea kabisa. Kilichobaki kwenye baadhi ya maeneo jirani ni mabomba ya kutolea moshi, mabaki ya miti na magari yaliyoungua moto na kutelekezwa. Baadhi ya watu wanasema hawaifahamu tena mitaa na maeneo yaliyozunguka mitaa yao ambayo wamekuwa wakiifahamu kila siku katika maisha yao yote.
No comments:
Post a Comment