Wednesday, October 4

Manchester United yampiga marufuku Pogba kucheza kikapu


Marekani. Madaktari wa timu ya Manchester United wamempiga marufuku mshambuliaji wa timu hiyo kucheza mpira wa kikapu baada ya kuonekana akipambana uwanjani huku mapumzikoni kutokana na kuwa majeruhi.
Mchezaji huyo alipelekwa Marekani kwa ajili ya matibabu zaidi kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya misuli. Drogba aliamua kuanza kucheza kikapu akiwa na lengo la kujiweka fiti pasipo kupata ushauri wa madaktari wa timu.
Hata hivyo, uongozi wa klabu hiyo umemwamuru kuacha mara moja kucheza mpira wa kikapu kwa sababu analazimika kuruka juu ili kufunga, jambo ambalo linaweza kumuongezea matatizo.
Mchezaji huyo amekuwa na mashabiki wengi nchini Marekani upande wa soka na mpira wa kikapu.

No comments:

Post a Comment