Tuesday, October 24

Cristiano Ronaldo afuta rekodi ya Messi


Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia huku kocha wake, Zinedine Zidane akitunukiwa kuwa kocha bora.
Ronaldo alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mwaka tuzo inayotambuliwa na Shirikisho la Soka la Dunia (Fifa), huku mshambuliaji wa Arsenal, Oliver Giroud akibeba tuzo ya Puskas kutokana na kufunga goli bora.
Ushindi wa Ronaldo umetokana na msimu uliopita kuisaidia klabu yake kutetea tena taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Pia, nyota huyo wa Real Madrid aliisaidia timu yake ya taifa ya Ureno kuibuka mabingwa wa Euro 2016 huku klabu yake ya Real Madrid ikitwaa ubingwa wa La Liga msimu uliopita.
Ronaldo aliwashukuru walompigia kura dhidi ya washindani wake Lionel Messi na Neymar.
Aliongeza kwamba “Wachezaji wenzangu, kocha, rais wangu, wote nawashukuru kwa ushirikiano wenu mlionipa miaka yote.”
Ronaldo sasa ameifikia rekodi ya mshambuliaji wa Barcelona, Messi ambapo wote kwa pamoja sasa wamechukua tuzo hiyo mara tano.

No comments:

Post a Comment