Wednesday, September 27

Wazazi wa Warmbier waeleza mateso yaliomkabili Korea kaskazini

Otto Warmbier asindikizwa na walinzi Korea kaskaziniHaki miliki ya pichaREUTERS
Wazazi wa Otto Warmbier wameelezea hali ya kutisha iliomkabili mtoto wao alipowasili nyumbani kutoka Korea kaskazini.
Fred na Cindy Warmbier wameliambia shirika la habari la Fox and Friends kuwa Watu wa Korea kaskazini ni "magaidi waliomtesa mtawalia" mtoto wao.
Mwanafunzi huyo wa Marekani alifungwa Pyongyang mnamo 2016 kwa kuiba kibandiko cha hoteli.
Aliachiwa kwa misingi ya matibabu mnamo Juni mwaka huu lakini aliwasili nyumbani akiwa mahututi na alifariki siku chache baadaye.
Korea kaskazini imekana daima kumtesa Warmbier. Inasema aliugua bakteria ya neva mwilini lakini madakatari wa Marekani hawakugundua bakteria yoyote.
'Hii haikuwa ajali'
Katika mahojiano yao ya kwanza tangu kufa kwake, wameliambia shirika la habari la Fox news kwamba "wanahisi umewadia muda kusema ukweli kuhusu hali iliyomkabili Otto".
Madakatari Marekani walisema alikuwa katika hali ambayo mwili wake ulikuwa hauitikii, lakini familia ya Warmbiers wanasema kuita hali hii coma "sio haki".
Bi Warmbier anasema walipomuona mtoto wao alikuwa "anazunguka na kufafatika kwa nguvu akitoa sauti isiyo ya binaadamu".
Kichwa chake kilikuwa kimenyolewa, alikuwa kipofu na kiziwi, mikono na miguu yake ilijipinda na alikuwana alama kubwa ya jeraha mguuni mwake, alisema. "Ilikuwa ni kama mtu ameyavunja na kuyapanga upya meno yake ya chini".
Picha ya February 29, 2016 Iliyochapishwa na Korean Central News Agency (KCNA) on March 1, 2016 inamuonyesha Otto Frederick WarmbierHaki miliki ya pichaAFP PHOTO / KCNA VIA KNS
"Otto aliteswa mtawalia na kwa kusudi na Kim na utawala wake. Hii haikuwa ajali," amesema bwana Warmbier.
Ameeleza kuwa mwanawe altengwa na familia yake, nchi yake, na dunia nzima nzima na kwamba serikali haikuwapa taarifa zozote kuhusu kifo chake.
Familia hiyo ilikataa afanyiwe upasuaji kubaini chanzo cha kifo kwasbabau wanasema walidhani kwamba ameteseka vya kutosha na "singeruhusu aondoke mbele ya macho yangu," aliongeza
Ametoa wito kwa watu wasiende Korea kaskazini ,akieleza ni kuchezea propaganda za Pyongayang. Raia wa Marekani wamepigwa marufuku sasa kusafiri kwenda Korea kaskazini.

No comments:

Post a Comment