Wednesday, September 27

Watalii 36 wakatiza likizo yao Afrika Kusini baada ya kuporwa mali yao

Afrika Kusini
Image captionAfrika Kusini
Kundi ya watalii kutoka nchini uholanzi wamesitisha likizo yao ya siku 22 nchini Afrika Kusini baada ya kuvamiwa na kuporwa mjini Johannesburg.
Watalii hao 36 walikuwa wamewasili kwenye uwanja wa ndege wa OR Tambo siku ya Jumapili na walikuwa wakisafiri wakitumia basi kwenda kwa hoteli yao waliposimamishwa na mwanamume ambaye alidanganya kuwa polisi.
Kituo cha News24 kiliripoti kuwa walisimamishwa na gari la polisi na mwanamume ambaye alikuwa amevalia sare za polisi, ambaye alikuwa na watu watano walikuwa wamevaa nguo za kawaida.
Mkuu wa polisi Fikile Mbalula aliomba msamaha kwa ubalozi wa uholanzi kufuatia kisa hicho.
Bw. Mablula alichapisha video akikutana na watalii hao na kuahidi kuwa watu hao watakamatwa.

No comments:

Post a Comment