Msimu mpya wa wanawake 100 wa BBC umerudi kwa kishindo.
Mpaka sasa majina 60 ya kwanza yametangazwa, akiwemo mwana anga za juu wa Nasa Peggy Whitson, Rais Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia. msanii Tiwa Savage wa NIgeria na mchezaji soka wa England Steph Houghton.
Majina mengine 40 yataongezwa katika msimu huu mwezi Oktoba.
Makala haya ya kila mwaka - yanayoangazia masuala yanayowahusu wanawake kote duniani inahimiza wanawake mwaka huu kufanya mabadiliko.
Orodha hiyo inajumuisha pia mshairi Rupi Kaur, muathiriwa wa shambulio la tindi kali Resham Khan na mtumbuizaji Jin Xing.
Visa vinavyoonekana kutomalizika vya unyanyasaji, ukosefu wa usawa, na kutoonekana kwa wanawake katika nyanja nyingi za kijamii, kunasababisha hisia ya kutowezeshwa wanawake na inavunja moyo.
Kwahiyo mwaka huu tunawataka wanawake kutoa njia za kukabiliana na mambo hayo yanayochangia ukosefu wa usawa kwa wanawake.
Ikiwa ni mwaka wa tano, Wanawake 100 wa BBC itaangazia masuala manne: Kufika viwango ambavyo huonekana sio kawaida kwa wanawake, elimu kwa mwanamke, unyanyasaji mitaani, na ubaguzi katika michezo kwa misingi ya kijinsia.
Baadhi ya watu katika orodha hiyo ya wanawake 100 wa BBC watashirikiana katika miji minne tofuai katika wiki nne za Oktoba kuunda njia itakayonuia kuwasaidia watu na matatizo haya.
Wengine watatoa usaidizi na nasaha kutoka maenoe yao kote duniani.
Ili wanawake 100 ifaulu itakuwani kutokana na kwamba wanawake kote duniani wamesaidia kuunda uelewa wa vipi na kwanini matatizo haya yana uzito.
Kwasababu wamewasilisha fikra nzuri ambayo wameiona, au kwasababu wamewasilisha wazo lao wenyewe.
Na sio wazo tu - Wanawake 100 itakuwana midahalo kwenye redio, katika mitandao ikiwemo ya kijamii.
Suala la kufika viwango ambavyo huonekana sio kawaida kwa wanawake litashughulikiwa San Francisco, elimu kwa mwanamke litakuwa Delhi, unyanyasaji mitaani ni mjini London, na ubaguzi katika michezo kwa misingi ya kijinsia litashughulikiwa Nairobi.
Lakini mdahalo unastahili kuwa kote duniani na tunataka kusikia mchango wa wanawake kote duniani.
No comments:
Post a Comment